RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, imeanza
kufanyiwa kazi na Bunge na ndani ya siku nane zijazo, umma utajua ukweli wake.
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alikabidhi ripoti hiyo kwa Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, jana
bungeni, na kamati imeanza kazi mara moja. Kwa mujibu wa Ndugai, taarifa hiyo
ya CAG ina maoni kwa kila hadidu za rejea kama chombo hicho kilipoagiza wakati
ilipotoa kazi kwa mkaguzi huyo.

Aliitaka
kufanya kazi chini ya Kanuni za Nyongeza za Bunge pamoja na ile ya Haki, Kinga
na Madaraka ya Bunge katika kushughulikia suala hilo linalosubiriwa kwa hamu
baada ya mjadala wa muda mrefu nchini.
Ndugai
akimwakilisha Spika wa Bunge, Anne Makinda, alimkabidhi Zitto mbele ya baadhi
ya wajumbe wake ripoti hiyo pamoja na juzuu nne kubwa (viambatanisho) vya
kuhusu ripoti ya sakata hilo.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda alikabidhi ripoti hiyo kwa Ofisi ya Spika wiki iliyopita,
kabla ya jana Ndugai kuikabidhi kwa Kamati ya Zitto anayesaidiwa na Deo
Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa (CCM).
Akizungumza
baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto alisema atazingatia maelekezo ya Spika ili
kuhakikisha wanakamilisha kazi na mchakato mwingine wa kibunge uchukue nafasi
yake. Aliwaambia wanahabari baadaye kuwa kamati hiyo katika kushughulikia
ripoti hiyo, itafanya kazi zake kiuchunguzi, tofauti na inapofanya kazi
nyingine.
No comments:
Post a Comment