HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 18 November 2014

"INASIKITISHA" KUMBE TANZANIA KUNA WAZEE MIL 2.5 TU..!!!



TANZANIA ina jumla ya wazee milioni 2.5 ambao umri wao  ni kati ya miaka  60 na zaidi kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

Naibu Waziri wa Afya  na Ustawi wa Jamii Dokta  Kebwe Stephen Kebwe amesema hayo  alipokuwa akijibu swali laMbunge wa Rombo Bwana  Joseph Selasini  aliyetaka kujua Taifa lina wazee wangapi wenye umri wa  kuanzia miaka 60 na kuendelea na ina mikakati gani ya kuwatunza wazee hao.

Naibu Waziri Kebwe amesema  hivi sasa serikali imeweka  mikakati mbalimbali ya kuwahudumia wazee hao katika sehemu mbalimbali ikiwa ni  pamoja  na kutungwa kwa Sera ya Kitaifa ya Wazee ya mwaka 2003 ikiwa na madhumuni ya kumuwezesha mzee kupata na kutumia huduma muhimu  za kijamii ili aweze kuishi kwa usalama na heshima.

Amesema mkakati mwingine ni pamoja na kuwahuduma wazee wanaotunzwa katika makazi maalumu 17 ya Serikali na 24 ya mashirika ya dini hapa nchini.
Hawa ni Wazee ambao walifanya kazi kwa iliyokuwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki , hapa ni namna
walivyokuwa nawasotea madai yao Mahakama kuu.




Pia kutoa msamaha wa kodi ya majengo kwa nyumba wanazoishi wazee wenyewe na kutenga dirisha maalum kwa matibabu ya wazee katika vituo vya kutolea huduma za afya vinavyomilikiwa na serikali.

Aidha amesema Wizara yake inashirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo asasi za kijamii zinzosimamia maslahi ya wazee nchini pamoja na Asasi za kimataifa zinzojishughulisha  na maslahi ya wazee.

No comments:

Post a Comment