![]() |
|
Waamini wakisafisha Eneo la Kanisa Jipya
|
Mwinjilisti
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania KKKT Usharika wa Kabuku Raphael Shemjawa amewaomba wadau mbalimbali na
mashirika binafsi kujitoa kwa hali na mali kuwasaidia katika ujenzi wa Kanisa jipya
unaondelea ushirikani hapo.
![]() |
|
Kanisa linalotumika kwa sasa
|
Aidha
alisema kuwa kwa sasa jengo wanalo tumia ni dogo sana na limechoka kwakuwa
limejengwa muda mrefu mnamo mwaka 1984
kwa miti na limekuwa likifanyiwa ukarabati mara kwa mara jambo ambalo amesema
bado halijakuwa katika hali yakuridhisha nakusema inafikia wakati washarika
wanasali nje kwa udogo wakanisa hilo.
![]() |
|
Kanisa jipya
|
Sambamba na hayo mwinjilisti huyo pia amewashukuru
washarika kwakujitoa marakwamara katika shughuli za ujenzi wa kanisa hilo
nakuwataka kuwa na moyo huo huo wakujitoa katika shughuli za kumtumikia Mungu
nakusema Mungu atawabariki katika maisha nashughuli zao za kila siku.



No comments:
Post a Comment