Na Mwandishi Wetu Tanga
Mnamo wa tarehe 11 Novemba mwaka huu majira ya saa saba za
usiku huko kijiji cha Kwemazandu kata na tarafa ya Magoma Wilaya ya Korogwe mtu
mmoja mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 18 hadi
30 asiyefahamika jina wala makazi aliuawa
kwa kupigwa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za wizi wa mbuzi mmoja mali ya Daudi Abdallah umri wa miaka 47 mkazi wa Kwemazandu.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Frazzer Kashai amesema kuwa amesema hakuna mtu aliyekamatwa
kutokana na tukio tukio hilo la mauaji.
Sambamba
na hayo Kamanda Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote kufanya kazi au
biashara zinazoruhusiwa kisheria ambazo
zinaweza kuwapatia kipato kwa na kuacha
kabisa biashara haramu za madawa ya
kulevya ambayo yanamadhara makubwa kwa afya za watumiaji.
Aidha
jeshi la polisi mkoani hapa pia limewataka wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua wale wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu
badala yake wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
No comments:
Post a Comment