Na Mwandishi Wetu.TANGA
Jeshi
la Polisi mkoani hapa limekamata kiasi cha kilogram 116 ya madawa ya kulevya
aina ya mirungi ambayo bado thamani yake bado hakija fahamika ikisafirishwa kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.134
CWL aina ya mitsubishi ikitokea Arusha
kuelekea Dar es salaam na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Haji Hamisi umri
wa miaka 27 ambaye ni Kondakta wa gari hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Frazzer Kashai amesema tukio hilo
mnamo wa tarehe 9 Novemba mwaka huu majira ya saa 20:00 usiku huko katika kizuizi cha Polisi Mombo maeneo ya
Liverpool kata na tarafa ya Mombo Wilaya ya Korogwe alikamatwa mtuhumiwa
huyo ambaye ni mkazi wa Moshi Pasua.
Aidha kamanda Kashai wakati mtuhumiwa akikamatwa
Dereva wa gari hilo alifanikiwa kutoroka na mtuhmiwa amekiri kufanya biashara
hiyo ya Mirungi kwa lengo la kujipatia kipato.
Hata hivyo kamanda huyo amesema
mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa baada ya
upelelezi wa awali kukamilika na msako mkubwa dhidi ya dereva
huyo aliyetoroka zinaendelea ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment