MABAO Mawili
yaliyofungwa na Hassani Materema kunako dakika za 18 na 79 yalitosha kuweza
kuwapa ushindi timu ya African Sports wa Mabao 2-1 dhidi ya Villa Squad katika
mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa jana katika uwanja wa CCM Mkwakwani
jiji Tanga.
African Sports ndio ilikuwa
ya kwanza kuweza kupata bao lake katika dakika ya 18 ambalo lilifungwa na
Hassani Materema baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Villa Squad
kabla ya Villa Squad kusawadisha dakika ya 36 kupitia Omary Masha.
TImu zote zilikwenda
mapumziko zikiwa nguvu sawa ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo
timu zote ziliingia uwanjani hapo zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya
mabadiliko kwa baadhi wa wachezaji wake.
Wakionekana kujipanga
vilivyo,African Sports waliweza kuongeza wimbi la mashambulizi langoni mwa
Villa Squad na kufanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 79 ambalo likifungwa
na Hassani Materema.
No comments:
Post a Comment