Kutokana na jitihada zinazo endelea kufanywa za kuzua
nakutokomeza matukio ya kiuhalifu zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa
Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata kilo zipatazo 221kg za madawa ya kulevya
aina ya mirungi zikiwa zimehifadhiwa ndani ya frezer .
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Frasser kashai
amesema tukio hilo limetokea maeneo tofauti katika mkoa huu ambapo amesema
manamo tar21 novemba mwaka huu majira ya saa 03:00 usiku huko maeneo ya
Raskazone Kata ya Central Tarafa ya Ngamiani Kusini Wilaya ya Tanga Mjini nyumbani
mwa mtu mmoja alie fahamika kwa jina la Sambia Abdallah 25 almkutwa amehifadhi
bunda 130 za sawa na kg 30 za madawa ya kulevya aina ya mirungi.
Hata hivyo
kamanda ameendelea kwa kusema kuwa mnamo majira ya saa 02 usiku huko maeneo ya
barabara ya 8 Kata na Tarafa ya Ngamiani Kati Wilaya ya Tanga walikamatwa watu wawili mke na mume
waliofahamika kwa majina ya Doti Hamisi 46 na Jamila Sadiki 30 wakiwa na bunda zipatazo 91 ambazo niswa na
kg 91 wakiwa wamezihifadhi kwenye freezer ndani ya nyumba yao.
Aidha
kamanda amesema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani kujibu
mashtka mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
Sambamba na
hayo Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi wotde kujiepusha na biashara
haramu ya uuzaji wa madawa ya kulevya kwakua yana madhara makubwa sana
afya Za watumiaji wa dawa hizo.
Katika tukio lingine mtu mmoja alie fahamika kwa jina la
Elibariki Michael 46mkazi wa Vunila
Kilindi amekutwa akiwa amejinyonga kwakutumia kamba ya katani hadi kufa. Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wajeshi la
polisi moani Tanga Fresssar Kashai amesema tukio hilo limetokea mnamo
tar 22 novemba mwaka huumajira ya 08: asubuhi.
Hata hivyo
kamanda kasha amesema chanzo ah tukio hilo ni kutikana na ugumu wa maisha
aliokuwa nao marehemu.
No comments:
Post a Comment