HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 13 November 2014

“KIMATAIFA KIRAFIKI” UHOLANZI HOI KWA MEXICO, ARGENTINA NA BRAZIL ZASHINDA



STRAIKA wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela, amesheherekea kurejea kuichezea Mexico baada ya Miaka Mitatu kwa kufunga Bao 2 wakati Nchi yake ikiichapa Netherlands Bao 3-2 huko Amsterdam kwenye Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki.
Carlos Vela, ambae aliichezea Arsenal Mechi 64 kati ya 2008 na 2012, alifungiwa Miezi 6 na Mexico Mwaka 2010 na baadae mwenyewe aliamua kutoichezea Mexico.

Vela alifunga Bao lake la kwanza kwenye Dakika ya 8 na Holland, waliocheza bila ya Nahodha wao Robin van Persie, walisawazisha Dakika ya 49 kwa Bao la Wesley Sneijder.
Kisha Vela na Javier Hernandez ‘Chicharito’ wakaongeza Bao 2 katika Kipindi hicho cha Pili.
Netherlands, chini ya Kocha Gus Hiddinck aliechukua mikoba kutoka Louis van Gaal baada ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Julai, sasa wamefungwa Mechi 4 kati ya 5 walizocheza mwisho.
Mechi inayofuata kwa Netherlands ni ya Kundi A la EURO 2016 dhidi ya Latvia hapo Jumapili na kwenye Kundi hilo wapo Nafasi ya 3 baada ya kupoteza Mechi zao na Czech Republic na Iceland.
VIKOSI:
Netherlands: Krul; Van Rhijn, Veltman, Vlaar, Willems; Afellay, Sneijder, Blind; Robben, Huntelaar, Depay
Akiba: Cillessen, Vermeer, Van der Wiel, Wijnaldum, Bruma, De Jong, Fer, Narsingh, Promes, De Vriji

Mexico: Ochoa; Aguilar, Reyes, M. Herrera, Alanis, Aldrete; Vazquez, H. Herrera, Guardado; Vela, Hernandez
Akiba: Corona, Talavera, Ponce, Jimenez, Gonzalez, Corral, Gio Dos Santos, Dominguez, Jonathan Dos Santos, Venegas
REFA: Szymon Marciniak [Poland]

MATOKEO:MECHI NYINGINE
Jumatano Novemba 12         
Turkey 0 Brazil 4                 
Belgium 3 Iceland 1             
Norway 0 Estonia 1             
Netherlands 2 Mexico 3                 
Argentina 2 Croatia 1
++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment