DANIEL STURRIDGE: ARUDI MAZOEZINI LIVERPOOL!
Straika wa Liverpool Daniel Sturridge ameanza tena
Mazoezi tangu aumie Musuli za Pajani [Hamstring] Mwezi Agosti akiwa na Timu ya
Taifa ya England.
Sturridge,
ambae alifunga Bao 21 katika Mechi 29 za Ligi Msimu uliopita, alikaribia
kurejea Uwanjani Mwezi uliopita lakini akapata maumivu mengine Mguuni
yaliyomweka nje kwa kipindi kingine.
Bosi wa
Liverpool Brendan Rodgers anategemea Sturridge atakuwa fiti kucheza Mechi yao
inayokuja ya Ugenini ya Ligi Kuu England na Crystal Palace hapo Novemba 23.
Msimu huu,
Sturridge amecheza Mechi 3 tu za Ligi na kufunga Bao walipocheza Anfield Agosti
17 na kuifunga Southampton 2-1.
Kwenye
Msimamo wa Ligi Kuu England, Liverpool wapo Nafasi ya 11 wakiwa Pointi 15 nyuma
ya Vinara Chelsea na hawajashinda katika Mechi 3 zilizopita.
ANDRE SCHURRLE APUUZA RIPOTI ZA KUIHAMA CHELSEA!
Lakini
Schurrle mwenyewe ameibuka Mtandaoni na kudai bado ana Mwaka mmoja na Chelsea
na kuuzima uvumi huo.
Msimu huu,
Schurrle amecheza Mechi mbili tu kwa Dakika zote 90, zote za Capital One Cup,
na mara nyingi Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amemtaka Mchezaji huyo kuongeza
bidii.
NANI: ANAIFIKIRIA SPORTING LISBON TU NA SI KURUDI MANCHESTER UNITED!
Nani, Winga wa Manchester United ambae yuko kwao
Ureno akicheza na Sporting Lisbon kwa Mkopo wa Msimu mmoja, amesema licha ya
Mashabiki wengi wa Man United kumtaka arejee Old Trafford yeye anataka abakie
Ureno tu kwa vile yupo kwenye raha kubwa.
Baada ya
kudorora akiwa na Man United, tangu arejee kwao kuichezea Sporting Lisbon Nani
amelipuka na kuwa Mchezaji moto.
Alipohojiwa
kama atakatiza kucheza kwa Mkopo Sporting na kurejea Man United, Nani alijibu:
“Sidhani kama kipo kipengele cha aina hiyo. Ni suala la Watu wengine kuamua. Ni
safi kupata upendo wa Mashabiki wa Man United. Wanataka nirudi. Lakini hapa
nipo kwenye wakati mzuri. Nafikiria kuendelea tu hapa. Soka ndio lilivyo, Siku
moja unasifiwa, Siku nyingine unapondwa!”
LIGI KUU
ENGLAND
RATIBA:
**Saa za
Bongo
Jumamosi
Novemba22
1800
Chelsea v West Brom
1800
Everton v West Ham
1800
Leicester v
Sunderland
1800
Man City v
Swansea
1800
Newcastle v
QPR
1800
Stoke v
Burnley
2030
Arsenal v Man
United
Jumapili
Novemba 23
1630
Crystal Palace v Liverpool
1900
Hull v
Tottenham
Jumatatu
Novemba 24
2300
Aston Villa v Southampton
No comments:
Post a Comment