Watu hao wakiwa Hospitali ya
Rufaa Bombo
kwa matibabu
|
Na Rebeca Duwe.TANGA
Katika tukio lisilokuwa la kawaida watu wawili
wamejeruhiwa vibaya Mkoani hapa wakati wakitekeleza uhalifu wa kuvua Samaki kwa
kutumia baruti(Uvuvi Haramu) katika bahari ya Hindi.
Watu hao wakiwa Hospitali ya
Rufaa Bombo
kwa matibabu
|
Watu hao walijeruhiwa baada ya kulipukiwa na
baruti hiyo wakiwa baharini wanavua kwa njia ya Uvuvi haramu. Watu hao wamepoteza
baadhi ya viungo vya miili yao ambapo Hamisi Omari Kassim amekatika mkono wa
kulia na ameumia jicho la kulia na Adam Selemani Kapera amekatika mikono yote
miwili na kuumia macho yote mawili pia amekatika vidole vyote vine vya mguu
wake wa kushoto na ameungua kifuani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa
Polosi Mkoa wa Tanga Fresser Kashai amesema chombo kilichotumika katika tukio
hilo kimetamuliwa kwa namba TTA 315 anina ya Ngalawa ambapo majeruhi wote
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo.
Watu hao wakiwa Hospitali ya
Rufaa Bombo
kwa matibabu
|
Katika taarifa yake kwa Waandishi wa Habari
Kamanda Kashai amesema Jeshi la Polisi mkoani hapa linatoa wito kwa wananchi kutoa
taarifa kwenye vyombo vya usalama mara wanapowaona wavuivi wanaovua kinyume cha
sheria hasa kwa kutumia baruti kitendo ambacho kinaleta madhara makubwa kwenye rasilimali kama samaki, pia samaki
wanaovuliwa kwa baruti huwa na madhara makubwa kwa afya za walaji.
No comments:
Post a Comment