FIFA imetangaza Wagombea 10 kuwania Tuzo ya Puskas, Goli Bora la Mwaka, na upigaji Kura wake umeanza.
Magoli hayo 10 Bora yamependekezwa na Kamati ya Soka ya FIFA na Washabiki wanatakiwa wapige Kura kupitia Mitandao ya FIFA na France Football na Zoezi hili kufungwa hapo Desemba 1.
Siku hiyo hiyo Desemba 1, Magoli Matatu Bora yatangazwa na Washabiki kupewa Nafasi nyingine kupigia Kura Goli Bora ambalo litashinda Tuzo ya Puskas na Mshindi kutangazwa Januari 12 Siku ambayo pia Mshindi wa FIFA Ballon d’Or, Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, atatangazwa.
Tuzo ya Puskas, Goli Bora la Mwaka, ilianzishwa kumuenzi Lejendari Ferenc Puskás, Nahodha wa Timu ya Taifa ya Hungary katika Miaka ya 1950.
Hii itakuwa ni mara ya 6 kwa Tuzo hii kutolewa.
Kwa kuyaona Magol hayo 10 na kupiga Kura BOFYA HAPA:
http://www.fifa.com/ballon-dor/puskas-award/index.html
TUZO YA PUSKAS
WAGOMBEA 10:
Tim Cahill – 18 Juni 2014, Australia v. Netherlands, 2014 FIFA World Cup™
Diego Costa – 23 Novemba 2013, Atlético Madrid v. Getafe, Primera División (Spain)
Marco Fabian – 15 Februari 2014, Cruz Azul v. Puebla, 1a División 2014 Clausura (Mexico)
Zlatan Ibrahimovic – 19 Oktoba 2013, Paris St. Germain v. SC Bastia, Ligue 1 (France)
Pajtim Kasami – 21 Oktoba 2013, Crystal Palace v. Fulham, Premier League (England)
Stephanie Roche -20 Oktoba 2013, Peamount United v. Wexford Youths, BEWNL (Rep.Ireland)
James Rodriguez – 28 Juni 2014 – Colombia v. Uruguay, 2014 FIFA World Cup™
Camilo Sanvezzo – 6 Oktoba 2013 – Vancouver Whitecaps v. Portland Timbers, MLS (USA/Canada)
Hisato Sato – 8 Machi 2014 – Sanfrecce Hiroshima v. Kawasaki Frontale, J.League (Japan)
Robin van Persie – 13 Juni 2014 – Spain v. Netherlands, 2014 FIFA World Cup™
No comments:
Post a Comment