Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart
Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland
itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane.
Akizungumza Dar es Salaam, jana (Novemba 5 mwaka
huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu saa 6
mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Katika
majina hayo 24, Nooij amemuita beki mkongwe wa zamani wa Yanga, Abuu Mtiro
ambaye sasa anakipiga Kagera Sugar.
Novemba 11 mwaka huu, Taifa Stars itaondoka kwenda
Afrika Kusini ambapo itaweka kambi ya siku mbili kabla ya kuondoka Novemba 13
mwaka huu kwenda Swaziland.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa
Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga). Mabeki ni Abubakar Mtiro
(Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan
Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua
(Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe
(Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni
(Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al
Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia),
Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga)
na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).
No comments:
Post a Comment