HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 5 November 2014

KWELI HUU MWAKA WAKE..!RONALDO ATWAA TUZO NYINGINE ULAYA.



Hapo jana  Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo amekabidhiwa Tuzo yake ya Buti ya Dhahabu kwa kuwa Mfungaji Bora kwenye Ligi za Bara la Ulaya na hii ni mara ya Tatu kwake kupata Tuzo hii.
Ronaldo ametwaa Tuzo hiyo kwa kupachika Bao 31 Msimu uliopita akiwa na Klabu yake Real Madrid akifungana na Luis Suarez ambae alifunga idadi hiyo hiyo ya Mabao wakati akiwa Liverpool.
Suarez, ambae sasa amehamia Barcelona, alikabidhiwa Tuzo yake hii mapema Mwezi uliopita.
Hii Leo, Ronaldo alikabidhiwa Tuzo yake na Rais wa Klabu yake Real Madrid, Florentino Perez, ambae alitamka Ronaldo sasa ni Lejendari wa Klabu hiyo kama alivyokuwa Alfredo Di Stefano.
Hii ni mara ya Tatu kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii, mara mbili akiwa na Real, na mara ya kwanza aliitwaa akiwa na Manchester United Mwaka 2008.
Msimu huu, Ronaldo tayari ameanza kwa moto mkali na tayari ana Bao 22.
Wiki iliyopita Ronaldo alitunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa La Liga na utitiri wa Tuzo hizi unamweka njia njema ya kutwaa tena Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, FIFA Ballon d’Or, ambapo Mshindi wake atatangazwa Januari 15.
****WASHINDI WALIOWAHI KUTWAA TUZO HIYO****

No comments:

Post a Comment