BINGWA MTETEZI WA AFCON (NIGERIA) AMEAIBISHWA NA SUDAN KWA KUCHAPWA GOLI 1-
Bingwa mtetezi wa kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), Nigeria, jana ameonja joto la jiwe baada ya kujikuta wakibanwa mbavu na Sudan kwa kuchapwa goli 1-0. Goli hili linaifanya timu ya taifa ya Nigeria chini kocha wa Stephene Keshi kuburuza mkia katika kundi lao lenye timu za Congo Brazaville na Afrika Kusini.
Sudan walipata goli la kwanza na
la ushindi mnamo dakika za mwisha wa kipindi cha kwanza ya mpepetano huo
kupitia mshambuliaji wao, Bakri Almadina
STARS YAMSHIKISHA ADABU BENIN KWA KUMCHARAZA MAGOLI 4-1 KAMA VILE WALIKUWA WAMESIMAMA
Nahodha wa Stars "Nadir Haroub Cannavaro (kushoto)akishangilia bao lake na Beki wa timu hiyo Oscar Joshua |
Watu wengi walikuwa wakiibeza sana Stars kuelekea katika mchezo wa jana dhidi ya Benin, lakini ndiyo hivyo Wahenga walisema, "mdharau mwiba, mguu huota tende" na ndicho kilichowakuta Wa Benin leo katika dimba la taifa licha ya kusheheni nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya kama vile, Stephane Sesegnon anayekipa kunako West Bromwich Albion.
Magoli ya Stars yalifungwa na
beki Haroub Canavaro, Amri Kiemba, Thomas Ulimwengu, pamoja naye Juma Luizio.
Goli la kufutia kijasho la Benin Lilifungwa na mshambuliaji Sadel akipokea pasi
maridadi kutoka kwake kiungo mshambuliaji, Stephane Sesegnon dakika ya 90 ya
mchezo huo.
Ushindi huo ni furaha kubwa kwa
watanzania ambao walikuwa wamekata tamaa na timu yao ya taifa iliyopo chini ya
kocho Mholanzi Mart Nooij kufuatia matokeo mabovu ya hivi karibuni katika
michuano ya kuwania tiketi za kupangwa katika makundi ya michuano ya AFCON yatakayo
fanyika mwakani nchini Moroco.
No comments:
Post a Comment