·
MTU mmoja aliyefahamika
kwa jina la Peter Simba mwenye umri wa miaka 45 mchunga Ngombe na mkaazi wa
kijiji cha Nyasa ameuawa kwa kukanyagwa shingoni baada kupigwa kwenye paji la
uso na mchunga Ngombe mwenzake aitwaye Modest Martin mwenye umri wa miaka 32
mkazi wa Nyasa.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Frasser Kashai
amesema lilitokea Oktoba tarehe 12 mwaka huu majira ya 4 asubuhi huko katika
kijiji cha Legazi Kata ya Nyasa Tarafa ya Magamba Wilaya ya Handeni.
Aidha kamanda Kashai
amesema chanzo cha mauaji hayo ni kugombea sehemu ya kunywesha mifugo na maiti
hiyo inafanyiwa uchunguzi na madaktari na itakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu
kwa ajili ya mazishi mara baada ya uchunguzi wa madaktari kukamilika.
Sambamba na hayo
kamanda Kashai amesema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu
mashtaka ya mauaji.
Jeshi la polisi mkoa
wa Tanga linatoa rai kwa wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuwafichua
wahalifu wote kwenye maeneo yao wanayoishi ili wananchi wema ambao ndiyo walio
wengi waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila usumbufu.
No comments:
Post a Comment