MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Omary Salim mwenye umri
wa miaka 42 mkazi wa Tanga na mlinzi wa kituo cha mafuta Lake Oil cha Kange
jijini Tanga ameuawa kwa kupigwa na nyundo kichwani kisha kuporwa silaha aina
ya shortgun yenye risasi mbili.
Katika tukio hilo
pia mlinzi mwingine Elisha Yohana mwenye umri wa miaka 48 mkazi wa Kange Kasera
amejeruhiwa kwa kupigwa sehemu mbali mbali za mwili na kisha kufungwa kwa
kamba.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani hapa, Frasser Kashai amesema
tukio hilo limetokea mnamo octoba 10mwaka
huu majira ya saa 8 usiku.
Majeruhi amelazwa
hospitali ya Bombo na hali yake inaendelea vizuri na msako na upelelezi wa
tukio hilo unaendelea
Katika tukio jingine…
Mwili wa mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Saida Salimu mwenye umri wa miaka 62 mkulima mkazi wa
Bumbuli umegundulika ukiwa umeharibika
baada ya kuuawa kwa kukatwa na panga mgongoni na mtu/watu wasiofahamika
wakati akiwa shambani.
Tukio hilo limetokea
Octoba 10 mwaka huu majira ya saa 1 jioni huko Mibuyu Mitatu Kitongoji cha
Buhosi Kata ya Mtindiro tarafa ya Muheza Wilaya ya Muheza.
Hata hivyo Kamanda
Kashai amesema kwamba mwili wa marehemu umezikwa na msako mkali wa kuwatafuta
waliohusika na mauaji hayo unaendelea.
No comments:
Post a Comment