Anayeelezwa
kuwa wakili wa Vilabu 12 Dk. Damas Ndumbaro
|
Shirikisho
la mpira wa miguu nchini Tanzania, TFF limemfungia Dr.Damas Ndombaro kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nje ya nchi ya Tanzaina kwa muda
wa miaka saba kwa sababu mbalimbali mojawapo ikiwa ni kupotosha klabu za ligi
kuu kuhusu makato ya asiliamia tano iliyotangazwa na TFF hivi
karibuni.
Baada
ya TFF kutangaza makato hayo klabu nyingi za ligi kuu kupitia mwanashria wao
Damas Ndombaru zilikataa kwa kishindo suala hilo huku zikitishia kugomea ligi
endapo TFF itapitisha makato hayo kwa nguvu. Makato ya asiliamia tano ambayo
TFF imetaka klabu zilipe zilikuwa zinatokana na wadhamini wa ligi ambao ni
Vodacom na Azam TV.
Makato
hayo yalikuwa yakilenga kusaidia soka la vijana wadogo ambao ndilo linaaminika
kuwa njia sahihi ya kupata wachezaji bora kwa ajili ya kusaidia nchi yetu
kisoka.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Jamal Malinzi
|
Inaaminika
kwamba Ndombaro alikuwa akipindisha baadhi ya vipengele vilivyopo katika katiba
ya bodi ya ligi ya tanzania ili kuwatetea wateja wake(klabu) wasikubaliane na
suala hilo, kitu ambacho ni kosa kisheria kufanya hivyo.
Wakili Dk.
Damas Ndumbaro ni mjumbe wa bodi ya ligi na mwanasheria wa kamati ya
uchaguzi ya klabu ya Simba
No comments:
Post a Comment