Madaraka Nyerere |
Familia ya baba wa taifa hayati
mwalimu Julius Kambarage Nyerere imeuomba uongozi wa benki kuu ya Tanzania
kuiondoa katika mzunguko wa fedha noti ya shilingi elfu moja yenye picha
ya Baba kwa maelezo kuwa picha ambayo imetumika katika noti hiyo haifanani
kabisha na kiongozi huyo na kwamba kuendelea kutumika ni sawa na kumdhalilisha
muasisi huyo wa taifa la Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya familia na
ukoo wa Baba wa taifa wakati wa kupokea mradi wa kuboresha makumbusha ya
Mwalimu Nyerere na kuzindua onesho la noti na sarafu ambazo zimetumika katika
vipindi tofauti kuanzia mwaka 1967 hadi sasa zenye picha na sahihi ya Baba wa
taifa, mmoja wa watoto wa Baba wa taifa Bw Madaraka Nyerere, amesema picha
iliyopo katika noti hiyo ya shilingi elfu moja haifanani na sura ya kiongozi
huyo hivyo kuomba benki hiyo kuangalia uwezekano wa kuiondoka katika mzunguko.
Naye kaimu gavana wa benki kuu ya
Tanzania Bw Juma Reli, pamoja na kutoa ahadi ya ukarabati nyumba ya kwanza ya
Baba wa taifa ambayo aliitumia kabla ya kujengewa na tanu amesema kuwa benki
hiyo imejitolea kuboresha makumbusho hayo ili kuhifadhia kumbukumbu zenye
histori ya baba wa taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wao mkurugenzi mkuu wa
shirika la makumbusho ya taifa Profesa Audax Mabula na mkuu wa wilaya ya
butiama Bi Angelina Mabula, wameishukuru benki kuu ya Tanzania kwa
kutambua umuhimu wa kuboresha makumbusho hayo katika kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali
za Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere ili kulinda historia za kiongozi huyo.(Chanzo ITV)
No comments:
Post a Comment