Askofu Titus Joseph Mdoe |
Na Dominic Maro.TANGA
WAKRISTU nchini wametakiwa kutambua chimbuko la
imani ya kweli ni familia iliyo na msingi bora na yenye furaha muda wote.
Rai hiyo imetolewa
na Askofu Titus Joseph Mdoe ambaye ni askofu msaidizi wa jimbo kuu la Dar es
salaam kwenye ibaada ya misa takatifu ya Hija ambayo imefanyika kwenye kituo
cha Hija Gare Lushoto jimbo Katoliki la Tanga.
Amesema familia
ndiyo chanzo na chimbuko la ukristu yatupasa kuimarisha familia zetu ilikuweza
kupata miito mbalimbali kama vile upadri,utawa,ndoa zilizo bora na taifa lenye
hofu ya Mungu.
Hata hivyo askofu
Mdoe hakusita kuomba maskofu, mapadre, makateksta na watawa kuwasaidia
wanafamilia wenye mgogoro kujua ukweli juu ya changa moto za familia ili
kuziponya.
Pia ibaada hiyo ya
Hija imehudhuriwa na maskofu wawili wakiwemo Askofu Mdoe na askofu Banzi ,
mapdre zaidi ya 35 , masister, makatekista na waumini zaidi 9000 kutoka kila
kona ya jimbo la Tanga na jirani.
No comments:
Post a Comment