Askari wa Jangwani (Simon Msuva na
Mbuyu Twite)
|
Kiingilio cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Simba it akayochezwa Jumamosi (Oktoba 18
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 7,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni wale
watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika
uwanja huo wenye viti 57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya
rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Askari wa Wekundu wa Msimbazi (Haruna Chanongo na
Ramadhani Singano Messi)
|
Tiketi zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za
elektroniki, na zimeanza kuuzwa jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana
kwa mtandao wa M-PESA, CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo
yapo zaidi ya mia moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo namba 27 itakayochezeshwa na
mwamuzi Israel Mujuni Nkongo akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha
itaanza saa 10 kamili jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka
mkoani Kilimanjaro.
Washabiki wanatakiwa kununua tiketi mapema,
kwani hazitauzwa uwanjani siku ya mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa
Mbagala (Uwanja wa Ndani) itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi
kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari maalumu tu yenye stika ndiyo
yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa kupitia Barabara ya Mandela. Pia
washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na
mabegi makubwa. Barabara ya kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa
watumiaji wa magari.
No comments:
Post a Comment