Kiongozi wa
Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler (1889-1945)
|
Na
Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
Kiongozi
wa Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler (1889-1945)
alikuwa mmoja kati ya Madikteta dhalimu na mwenye nguvu kuwahi kutokea katika
karne ya 20.
Baada ya
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mbabe huyo aliamkakwa nguvu kupitia Chama hiko cha
Wafanyakazi wa Ujerumani na kuchukua udhibiti wa Serikali ya Ujerumani mnamo
mwaka 1933.
Hitler
aliamuru uanzishwaji wa kambi za mateso dhidi ya Wayahudi na makundi ya watu
wengine huku akiamini kuwa kufanya hivyo ilikuwa
chachu na tishio tosha dhidi ya ukuu wa himaya ya Aryani na hatimaye
kusababisha vifo vya zaidi ya Wayahudi wapatao milioni Sita.
Mashambulizi
ya Ujerumani dhidi ya nchi ya Poland mwaka 1939 ndiyo yaliyoanzisha Vita Kuu ya
Pili ya Dunia ambapo mpaka kufikia mwaka 1941Ujerumani iliteka sehemu kubwa ya
ardhi ya Ulaya na Afrika Kaskazini.
Ili
kuepuka kukamatwa kwa kukwepa utumishi katika jeshi la Austria-Hungary, Adolf
Hitler aliondoka toka Vienna na kuelekea Munich mnamo Mei 1913 lakini baadaye
alilazimika kurudi tena.
Taarifa za
kihistoria zinasema kuwa Kiongozi huyo wa Nazi alijiunga na jeshi la Bavaria na
kuanza kufanya kazi za kujitolea ambapo mwaka uliofuata alishiriki kikamilifu
katika vita ya Kwanza ya Dunia akiwa mstari wa mbele upande wa Magharibi ambapo
uzoefu wake katika vita na mapambano uliathiri mawazo, fikra na mitazamo yake
yote baada ya hapo.
Baada ya
Vita Kuu ya kwanza ya Dunia, Hitler alichukua udhibiti wa chama hiko cha
wafanyakazi wa Ujerumani kama kiongozi hivyo alitumaini kingemwezesha kushika
dola ya Ujerumani punde si punde.
Aliposhindwa
kwenye jaribio la Mapinduzi la mwaka 1923 yeye na wenzake walikamatwa na
kufungwa jela na baada ya kutoka jela alijitahidi kukijenga chama hiko na
kuanza mikakati ya kukamata dola kwa njia zilizo halali.
Hitler
alikusudia kufanya mageuzi na kuendesha sera za kibaguzi ambazo zingetoa nafasi
ya kutosha kwa Wajerumani kuweza kuishi katika himaya kubwa duniani.
Kwanza
alitabiri ingekuwa rahisi kuiteka Czechoslovakia, na kufuatiwa na Ufaransa
ambayo ilikuwa kizingiti kigumu kwa wakati huo hatimaye kumalizia na nchi ya
Uingereza.
Kwa mujibu
wa mikakati ya Adolf Hitler, vita ya Tatu ingefuata juu ya uvamizi dhidi ya
Jumuiya ya Kisovieti ambayo kwake ulikuwa ni mtihani ambao alipanga afaulu kwa
kufikiri vita ingepiganwa kwa haraka na kwa urahisi.
Kwa mujibu
wa fikra zake za kuipiga Urusi, hii ingempa utajiri wa malighafi za kutosha
hususan mafuta ambayo yangemwezesha kuandaa mkakati wa maandalizi ya vita ya
Nne dhidi ya Marekani.
Vita hiyo
ingekuwa rahisi tu kwake endapo Ujerumani ingeweza kuwa na ndege ziwezazo
kusafiri masafa marefu pamoja na meli za kivita na kwa upande mwingine ndege za
kutosha na jeshi la maji kubwa na imara lingemwezesha kumkabili adui kokote
aliko bila umbali kuwa kikwazo.
Kiongozi wa
Chama cha Kisoshalisti kilichojulikana kama “NAZI” Adolf Hitler (1889-1945)
|
Mara baada
ya Hitler kuingia madarakani mwaka 1933, maandalizi ya Ujerumani kijeshi
yalianza kufanyika, hivyo mkazo na mkakati wa muda mfupi ulikuwa kutengeneza
silaha kwa ajili ya vita dhidi ya mataifa ya Magharibi na mkakati wa muda mrefu
ulikuwa juu ya uzalishaji wa silaha nzito kwa ajili ya vita dhidi ya Marekani.
Mnamo
mwaka 1938 Hitler aliachana na mpango wa uvamizi wa kijeshi dhidi ya
Czechoslovakia na kuangalia zaidi makubaliano ya amani na kiongozi wa nchi hiyo
ambayo yalifanyika mjini Munich na hilo lilikuwa kosa lake baya na kubwa kuwahi
kulifanya.
Alipoamua
kuigeukia Ufaransa na Uingereza Hitler hakuweza kuishawishi Serikali ya Poland
kujiunga na kuwa sehemu ya himaya ya Ujerumani kwa njia za amani ili
kuhakikisha hali ya utulivu inakuwepo katika Mashariki ya Ulaya, hivyo
alichukua maamuzi ya kuivamia na kuiharibu Poland kabla ya kuanza kuzikabili
nchi za Magharibi.
Uvamizi wa
nchi ya Poland ulikususudiwa kufanyika ifikapo Septemba 1, 1939 lakini, ili
kufanikisha adhma yake hiyo na ushindi wa haraka juu ya Poland kwa kuvunja kila
aina ya kikwazo mbele yake, alikusudia kuiingiza Ujerumani katika makubaliano
na Urusi ili mwisho wa siku iwe rahisi kwake kuzivamia nchi za Magharibi bila
pingamizi lolote baada ya Poland.
Hali
kadhalika, Hitler alikusudia kufanya uvamizi dhidi ya Mataifa ya Magharibi
katika msimu wa baridi mwishoni mwa mwaka 1939, lakini hali mbaya ya hewa
ilikuwa ni kikwazo kikubwa ambacho kingeathiri jeshi lake la anga,
kwahiyo aliamua kuhairisha mpango huo na kuhamishia uvamizi huo ifikapo
mwanzoni mwa mwaka 1940 katika majira yajoto.
Kutokana
na ushauri alioupata toka kwa Admiral Erich Raeder juu ya kuivamia na kuiteka
Norway ili kuwezesha upatikanaji wa njia rahisi kwa jeshi lake la maji katika
bahari ya Atlantiki kuelekea Kaskazini, aliivamia Norway mwaka Aprili 1940.
Baada ya
kupokea ushauri tena toka kwa Kamanda Mkuu Erich Von Manstein lengo la uvamizi
kuanzia Kaskazini lilibadilishwa na kuamua kupanga mashambulizi kuelekea nchi
zilizoko Kusini mwa Ulaya kwa lengo la kuzuia misaada ya kijeshi toka jeshi la
Washirika (Allied force) kuelekea nchi za Ubelgiji na Uholanzi.
Mkakati
mpya wa Hitler kwa mara ya kwanza ulionekana kufanya kazi wakati jeshi la
Ujerumani lilipofanikiwa kuvunja mstari wa ulinzi wa jeshi la Kifaransa na
kufanikiwa ndani ya siku kumi kufika kwenye mkondo wa pwani nyuma ya vikosi vya
majeshi ya Muungano.
Baada ya
kuonekana wazi kuwa majeshi ya Washirika yaliyokwama yanaweza kutotoroka kipigo
cha jeshi la Ujerumani, mwelekeo wa silaha na jeshi la Ujerumani ulibadilika
tena, lakini jeshi hilo lilikwisha chelewa kuweza kuzuia na kufanya
mashambulizi dhidi ya askari wa jeshi la Muungano kwasababu kikosi maalumu cha
jeshi la Uingereza na wanajeshi wa Ufaransa walifanikiwa kuokolewa na kutoroka.
Pigo
lililotokea mapema mwa mwezi Juni 1940 lililopelekea anguko kwa mstari wa
mwisho wa ulinzi wa jeshi la Ufaransa ulikuwa ni ushindi kamili uliompa Hitler
furaha na shangwe huku akijua anapata msaada wa kutosha toka kwa Makamanda na
Majemedali wake wa kivita, ambao kila mara alikuwa akiwapandisha vyeo na kuwapa
namna nyingine za rushwa kama sehemu ya kuwapa motisha ya kuendelea na
mapambano.
Taarifa
zinasema kuwa, kwasababu ilionekana kama vita hii ilikuwa imeisha baada ya
Ujerumani kuiteka Ufaransa, Hitler alianza kupanga mipango mingine kwa ajili ya
vita dhidi ya Marekani na Umoja wa Kisovieti.
Mnamo
Julai 11, 1940 Hitler alitoa amri kuanza kwa ujenzi wa jeshi la maji ikiwemo
ujenzi wa meli za kivita na ilipofika Julai 31, 1940 baada ya mkakati wa kutaka
kuvamia Umoja wa Kisovieti katika msimu wa baridi wa 1940, Hitler kutokana na
ushauri wa wafanyakazi wake wa kijeshi aliamua kuishambulia Urusi katika majira
ya joto mwishoni mwa mwaka1941.
Wakati Uingereza
ikikataa kukubali kushindwa na kusalimu amri, Hitler alipanga kuchanganya hatua
tatu ambazo zingehakikisha Uingereza inasalimu amri;- Kwanza kabisa, jeshi la
anga la Ujerumani lingefanya uvamizi na kuharibu uwezo wa Uingereza kujitetea;
Pili Uingereza ingevamiwa ardhini iwapo kama isingejisalimisha, na tatu ushindi
ambao ungepatikana dhidi ya Urusi ungeondoa uwezekano wa Uingereza kupata
msaada wowote ule toka Urusi, hivyo kuangamia zaidi na kumaliza hatari yoyote
dhidi ya Japan, ambayo ingehamasika kusafiri katika bahari ya Pasifiki na
kuivamia Marekani upande wa Magharibi.
Kwa upande
mwingine Hitler alitaka Japan kujiunga katika vita na Uingereza na kuahidi
kujiunga na Japan katika vita dhidi ya Marekani kama Tokyo ingeona umuhimu juu
ya hilo, na hii ingekuwa njia nyingine kwa Ujerumani kupata kuimarisha jeshi la
maji dhidi ya Marekani.
Kampeni
dhidi ya eneo la Balkan, kiongozi huyo mbabe wa enzi hizo (Hitler) alikusudia
kupata alicho amini kuwa ngome ya upande wa Kusini iliyokuwa katika hali tete
lakini hata hivyo aliona operesheni kubwa ya jeshi la anga katika eneo la
Balkani ingekuwa ya gharama ya juu sana kutokana na ugumu wa eneo lenyewe na
hivyo kutokusudia kufanya operesheni kama hiyo tena.
Ikumbukwe
kuwa, uvamizi wa Ujerumani dhidi ya Umoja wa Kisovieti, ulianza tarehe 22 Juni,
1941 ambapo hapo mwanzo uvamizi huo ulionekana kwenda kama ilivyo pangwa,
lakini gafla kila kitu kilianza kwenda vibaya vipigo vya kwanza ambavyo
vilikusudia kuangusha Umoja wa Kisovieti ndani ya wiki chache havikuleta
matokeo yaliyokusudiwa na hayakuweza kuwa na athari katika nchi hiyo, hivyo
baada ya hapo, swali daima lilikuwa kwa Ujerumani ni sekta ipi nyeti na muhimu
ishambuliwe ili kuidhoofisha Urusi na sekta gani iachwe.
Katika
hali hiyo, Hitler alijikuta mara kwa mara akitofautiana na Majenerali
wake walioko mstari wa mbele katika kuamua mustakabali wa vita na baada ya vita
kuonekana ikiielemea na kuigeukia Ujerumani hali ya kutofautiana kati ya
Makamanda wa Hitler ilizidi kuongezeka.
Wakati
jeshi la Ujerumani likiendelea kurudi nyuma, Hitler alikuwa daima na wasiwasi
kuhusu hasara waliyokuwa wakiendelea kuipata ya watu hali kadhalika ya
uharibifu wa vifaa vyake vya kijeshi kwahiyo baadhi ya Majemadari kama Erwin
Rommel na Walther Model, mara kwa mara walikuwa wanapingana na amri ya Hitler
kwa kurudi nyuma wakati Majenerali wengine walikuwa wakirudishwa nyumbani
kukusanya kiinua mgongo chao cha kila mwezi na kustaafu kwa kutofautiana na
amri za kiongozi wao ingawa wengine walikuwa wakiendelea na kazi zao.
Hitler
alifikiri kwamba kushindwa kwa Ujerumani katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
kulitokana na anguko lililotokea katika ardhi ya nyumbani mbele na kwa hivyo
kudhani kuwa uanzishwaji wa sera za kidikteta na mauaji ya kukusudiwa ya Wayahudi
ulikuwa uhakika wa ushindi wa vita dhidi ya majeshi washirika na safari hii
Hitler alipoona hana jinsi na majeshi washirika yameshaingia mjini Berlin huku
yakiongozwa na Jeshi Jekundu la Urusi, Hitler alijawa na hofu ya kisasi ambacho
Warusi wangetoa dhidi ya Wajerumani, hivyo aliamua kumuoa mke wake na wote kwa
pamoja kuamua kujiua muda mfupi kabla ya jeshi la Urusi kuwasili.
(Makala imeandaliwa na Benedict
Liwenga kwa msaada wa mtandao)
No comments:
Post a Comment