Kikosi cha African Sport wana “Kimanumanu”
|
Kikosi cha Lipuli FC
|
Na Godwin Henry. TANGA
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza
FDL msimu wa 2014/15 imeendelea hapo jana ambapo katika Dimba la CCM Mkwakwani hapa
jijini Tanga wawakilishi wa Mkoa wa Tanga katika ligi hiyo African Sport “wana
kimanumanu” walishindwa kutamba katika Uwanja wao wa nyumbani na kulazimishwa
sare ya 1-1 dhidi ya Lipuli FC ya Iringa.
Katika mchezo huo bao la Sport
lilipatikana mnamo dk ya 44 ya kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penalt
uliopigwa na kiungo Ali Ramadhani “Kagawa” kufuatia madhambi yaliyofanywa na
walinzi wa Lipuli dhidi ya Mshambuliaji wa Sport katika eneo la hatari.
Bao
la kusawazisha la Lipuli lilipatikana mnamo dk ya 54 likifungwa kiufundi na
Winga Musa Abdallah kufuatia uzembe uliofanya na Beki wa kushoto wa African Sport
"Mwita Gereza"kushindwa kumiliki mpira vizuri alionziwa na Golikipa wao Yusuph Yusuph.
Katika mchezo huo Sport walionesha ufundi wa wa hali ya juu kwa kutandaza soka la pasi nyingi fupifupi na kufanikiwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo walishindwa kuzitumia.Winga wa African Sport Maulid Abbas alieingia kipindi cha pili alionesha kipaji cha hali ya juu kwa chenga za maudhi na krosi za uhakika.
Nao Lipuli hawakuwa nyuma kwani walitumia mipira mirefu na kushambulia kwa kasi ambapo mara kadhaa walijikuwa wako na golikipa lakini bahati haikuwa yao kwani umaliziaji ulikuwa dhaifu sana.
Kikosi cha Sport
jana kilikuwa na
1.Yusuph
.A.Yusuph GK
2.Mwaita
Gereza
3.Ali
Isa Ali
4.Juma
Shemvuni
5.Nzara
Ndaro
6.Mussa
Mohammed
7.Mohammed
Issa
8.Ali
Ramadhani
9.Hasaan
Matarema
10.Hussein
Issa
11.Evarigestus
Munjwahuki
Sub
1..Zakaria Mwaluko GK
25.Khalfan Kwenye
15.Issa Shabani
05.James Salu Mondi
12.Maulid Abbas "dk 60'
09.Fadhil Abdallah Kizenga
26.Maulid Milanda
Africna Sport watakuwa tena Dimbani
Jumapili Oct 19 kuwakabili Polisi ya DSM katika Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga, Mchezo utakaoanza saa 10 kamili za jioni.
No comments:
Post a Comment