Mfano |
Na Evelyn Balozi.TANGA
JESHI la polisi mkoani
hapa linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Charles 28, mkazi
wa Morogoro kwa kupatikana na risasi moja ya shortgun na 38 za Markfour zikiwa
ndani ya begi lake.
Mtu huyo amekamatwa eneo la maili Kumi Kata
ya Segera Tarafa ya Mkumburu Wilaya ya Korogwe ya basi la abiria No.T.510 CLB
aina ya Nissan Caravan akitokea Monduli mkoa wa Arusha kwenda mkoani Morogoro.
Katika tukio hilo la Octoba 8 mwaka huu
majira ya 5 usiku mtuhumiwa amekiri kufanya biashara hiyo ya usafirishaji wa
risasi na alieleza kuwa risasi hizo ameagizwa na mkazi mmoja wa Mkoani
Morogoro.
Wakati huohuo Jeshi la polisi Mkoani hapa
linawashikilia Keneth Ekenee 31 na Ameki Boniface 31 raia wa Nigeria kwa kumiliki
milipuko 8 ya miamba ya madini pamoja na waya mmoja wa kuunganisha milipuko
hiyo.
Kamanda Kashai amesema tukio hilo limetokea Octoba
12 mwaka huu majira ya saa saba mchana huko kijiji cha Kigwashi Kata ya Mashewa
Tarafa ya Magoma Wilaya Ya Korogwe ambapo watuhimiwa hao wakiwa nyumbani kwa
mwenyeji wao aitwaye Frenk maarufu Miki ambaye alikimbia mara baada ya
watuhumiwa hao kukamatwa.
No comments:
Post a Comment