JUMAMOSI, Uwanja wa Taifa Jijini Dar
es Salaam utarindima kwa Dabi ya Kariakoo wakati Vigogo wa Soka Nchini Tanzania
na Watani wa Jadi, Yanga na Simba,watakapovaana katika pambano lao la kwanza
la Ligi Kuu Vodacom kwa Msimu wa 2014/15.
Watani hao wanatinga kwenye kimbembe
hiki kinachongojewa Nchi nzima hasa kwa vile Msimu huu kila Timu ina Benchi la
Ufundi jipya kwa Yanga kuwa na Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania
kutoka Brazil Marcio Maximo, na Simba kuongozwa na Kocha wao wa zamani Mzambia
Patrick Phiri.
Vile vile mvuto zaidi ni ule wa
kuona Wabrazil wa Yanga, Kiungo Andrey Ferreira Coutinho na Geilson Santos '
Jaja' wakivaana na Simba iliyomteka Straika wa Yanga, Mganda Emmanuel Okwi.
Hii itakuwa Mechi ya 4 ya Ligi kwa
kila Timu lakini Yanga wanaingia wakiwa Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 6 wakati
Simba wako Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 3.
Msimu huu, Yanga walianza kwa
kuchapwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Morogoro na kisha kushinda Mechi mbili
mfululizo dhidi ya Ruvu JKT na Prisons, zote kwa Bao 2-1 kila moja.
Simba wao hawajafungwa lakini
hawajashinda hata Mechi moja katika Mechi 3 walizocheza kwa kutoka Sare na 2-2
na Coastal Union na Sare za 1-1 dhidi ya Stand United na Polisi Morogoro.
++++++++++++++++++++++++++
VIINGILIO:
-Viti Bluu na Kijani: Sh 7,000 [Viti
36,693]
-Viti Chungwa: Sh 10,000
-Viti VIP B na C: Sh. 20,000
-Viti VIP A: Sh. 30,000
**Jumla Viti 57,558
**Tiketi Elektroniki zitauzwa
M-PESA, CRDB Simbanking na Maduka ya CRDB Fahari Huduma.
**TIKETI HAZITAUZWA UWANJANI SIKU YA
MECHI
++++++++++++++++++++++++++
Hivi sasa kila Timu imejichimbia
kwenye Mazoezi makali kwa Simba kukimbilia huko Afrika Kusini na Yanga kubakia
Jijini Dar es Salaam wakifanya Mazoezi yao Uwanja wa Boko Veterani.
Katika Misimu miwili iliyopita,
Matokeo katika Dabi ya Kariakoo ni 1-1 Msimu wa 2012/13 na Yanga kushinda 2-0
Mechi ya Marudiano na Msimu wa 2013/14 kutoka Sare Mechi zote mbili za Bao 3-3
na kisha 1-1.
++++++++++++++++++++++++++
>>ONYO KALI: Mashabiki
hawaruhusiwi kuingia Uwanjani wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi
makubwa
>>BARABARA: Barabara ya
kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.
++++++++++++++++++++++++++
Nahodha wa Simba Joseph Owino
|
Refa wa mtanange huu wa Jumamosi ni
Israel Nkongo ambae atasaidiwa na Ferdinand Chacha na John Kanyenye wakati
Hashim Abdallah atakuwa Refa wa Akiba na Kamishna ni Salum Kikwamba.
Msimu uliopita, Refa Israel Nkongo
ndie aliesimamia Mechi ya Mahasimu hawa ambapo Yanga waliongoza 3-0 hadi
Mapumziko na Simba kuweza kurudisha na kupata Sare ya 3-3.
Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri
|
Vikosi:Simba
Makipa:Hussein
Sharrif ‘Cassilas’, Ivor Mapunda,Manyika Peter
Mabeki:Nassor Masoud
‘Chollo’William Lucian ‘Gallas, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka,
Joseph Owino,Joram Mgeveke
Viungo:Jonas Mkude,
Ramadhani Singano ‘Messi’, Pierre Kwizera,Shaban Kisiga,Haruna Chanongo.
Washambuliaji:Amisi
Tambwe,Elias Maguri , na Emmanuel Okwi.
Mfumo:4:1:3:2
Kocha
wa Yanga Mbrazil Marcio Maximo(kushoto)
|
YANGA
Makipa: Deo Munishi "Dida", Juma
Kaseja na Ally Mustafa "Barthez"Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Mbuyu Twite, Omega Seme, Hassan Dilunga, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima na Said Juma "Makapu" Coutinho
Washambuliaji: Said Bahanuzi, Hussein Javu, Hamis Kizza, Geilson Santos "Jaja", Saimon Msuva na Mrisho Ngasa, Tegete
Mfumo:4:4:2
Nahodha
wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro
|
RATIBA:
Jumamosi Oktoba 18
Polisi Moro v Mtibwa Sugar
Ndanda FC v Ruvu Shooting
Kagera Sugar v Stand United
Coastal Union v Mgambo JKT
Mbeya City v Azam FC
Yanga v Simba
Jumapili Oktoba 19
Prisons v JKT Ruvu
MSIMAMO:
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Mtibwa Sugar
|
3
|
3
|
0
|
0
|
6
|
1
|
5
|
9
|
2
|
Azam FC
|
3
|
2
|
1
|
0
|
5
|
1
|
4
|
7
|
3
|
Yanga
|
3
|
2
|
0
|
1
|
4
|
4
|
0
|
6
|
4
|
Mbeya City
|
3
|
1
|
2
|
0
|
1
|
0
|
1
|
5
|
5
|
Tanzania Prisons
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
2
|
1
|
4
|
6
|
Kagera Sugar
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
2
|
1
|
4
|
7
|
Coastal Union
|
3
|
1
|
1
|
1
|
4
|
4
|
0
|
4
|
8
|
Stand United
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
5
|
-2
|
4
|
9
|
Ndanda FC
|
3
|
1
|
0
|
2
|
6
|
6
|
0
|
3
|
10
|
Simba
|
3
|
0
|
3
|
0
|
4
|
4
|
0
|
3
|
11
|
Mgambo JKT
|
3
|
1
|
0
|
2
|
1
|
2
|
-1
|
3
|
12
|
Polisi Moro
|
3
|
1
|
1
|
1
|
3
|
5
|
-2
|
2
|
13
|
JKT Ruvu
|
3
|
0
|
1
|
2
|
1
|
4
|
-3
|
1
|
14
|
Ruvu Shooting
|
3
|
0
|
1
|
2
|
0
|
4
|
-4
|
1
|
No comments:
Post a Comment