Dimbwi kubwa la maji machafu yakiwa na takataka nyingi lililoko katika barabara ya Misufini kijijini hapo "Picha hii imepigwa leo" |
Wakazi wa Kijiji cha Pongwe kaskazini kilichoko Kata na Tarafa ya Pongwe Jijini Tanga wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho chini ya M/kiti wake Mzee John Mpanje kwa kushindwa kutatua kero ya Dimbwi kubwa la maji machafu lililoko katika barabara ya Misufini kijijini hapo.
Wakizungumza na Redio Huruma fm wakazi hao wamesema wamewahi kufikisha taarifa hizo mpaka kwa Uongozi wa Kata hiyo inayoongozwa na Diwani Mwana Uzia(CCM) ,ambapo hawakupata ufumbuzi na badala yake wamekuwa wakipewa ahadi pasipo utekelezaji.
Akizungumza na Kituo hiki mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Michael Chikoma amesema Dimbwi hilo limekuwapo kwa muda sasa na hali huwa mbaya zaidi wakati wa kipindi cha Mvua.
Barabara hiyo mbali na kutumiwa na wakaazi wa kijiji hicho pia Malori yanayonena Mawe kutoka Mkurumuzi huitumia kama njia kuu na pia inaunganisha wakazi wa maeneo jirani ya Kijiji cha Pingoni kilichopo kata ya Maweni, Chote na Pande.
Kufuatia malalamiko hayo Mwandishi Wetu alilazimika
kumtafuta kwa nja ya simu Diwani wa Kata hiyo Mwana Uzia ambapo alisema kuwa
yuko kwenye kikao hivyo hakuweza kuzungumza chochote.
Hata hivyo bado Mwandishi wetu anaendelea kuwa
tafuta wahusika zaidi ili kubaini uzito wa jambo hili unatokana na nini.
No comments:
Post a Comment