Na Rebeca Duwe Tanga.
Jeshi la polisi mkoani Tanga
linamshikilia mtu mmoja aliefahamika kwa jina la Huseni Said mwenye umri
wa miaka 24 aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba za usajili T .745 CGK kwa kosa la kuwagonga watu wawili waliokuwa
wakitembea kwa miguu na kusababisha vifo na majera.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
hapa Frasser Kashai amesema mnamo tarehe
17 oktoba mwaka huu huko maeneo ya Kwamaligwa kata ya Kibirisha tarafa ya Mgera
wilaya ya Kilindi mkoani hapa Husein
Said mwenye umri wa miaka 24 ambye ni dereva wa pikipiki hiyo aliwagonga
watembea kwa miguu Kauye Mjwayu na
kufariki dunia mara baada ya kufikshwa zahati ya Kibirashi ambapo Rehema Said
mwenye umri wa miaka 24 naye aligongwa kuumia
bega la kulia wote wakiwa ni wakazi wa Kwamaligwa.
Hata hivyo kamanda Kashai amesema kuwa chanzo ajali hiyo ni mwendo kasi
ambapo mtuhumiwa amekamatwa na atafikshwa mahakamani mara upelelezi kukamilika.
Sanjari na hayo jeshi la polisi
linatoa wito kwa wananchi kuheshimu sheria za nchi, kwani kufanya kitendo
chochote kinyume cha sheria ni kosa na sheria itachukua mkondo wake.
Aidha ametoa wito kwa watumiaji
wote wa vyombo vya moto na watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria usalama
za usalama barabarani .
No comments:
Post a Comment