Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga
Frasser Kashai akizungumza na Waandishi wa habari.(hawapo pichani)
|
Na Rebeca Duwe.TANGA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Emanuel Lugazo 18 mkulima na mkazi
wa Chamwino Dodoma amefariki dunia mara baada ya kukatwa na mapanga kichwani na mkono wa kushoto na watu
wasiojulikana alipokuwa akilima shambani kwa Damian Aloyce 49 mkazi wa Kwamgwe
na kumuibia kiasi cha Tshs.300,000 pamoja na simu za mkononi 3 ambazo thamani
yake bado haijafahamika.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio hilo
limetokeo mnamo tarehe 18 oktoba mwaka huu majira ya saa 5 usiku huko Kwamgwe
Kata na Tarafa ya Mkumbuli Wilaya ya Handeni .
Sambamba na hayo Kamanda Kashai amesema chanzo cha mauaji hayo bado
kinachunguzwa na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na hivyo basi
msako wa kuwatafuta watuhumiwa unaendelea.
No comments:
Post a Comment