Na Rebeca Duwe TANGA
Jeshi la polisi mkoani hapa
linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Khalid Ramadhani 28, mkazi wa makorora kwa kosa la
kupatikana na noti bandia 11,kila noti
moja ikiwa na thamani ya Tshs.10,000 sawa na thamani Tshs.110,000 kwa noti
zote.mbali na noti hizo mtuhumiwa huyo pia amekutwa na noti bandia nne za dola
100 za Marekani.
Akithibitisha kutokea kwa
tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea
mnamo tarehe 19 octoba mwaka huu majira ya saa 10 jioni huko katika maeneo ya
Mikanjuni kata ya Mabawa Tarafa ya Ngamiani kati Wilaya ya Tanga mjini.
Aidha kamanda Kashai
amesema mtuhumiwa huyo amekiri kufanya biashara hiyo ya uuzaji wa noti bandia
na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment