Mbunge wa Korogwe vijijini
Profesa Maji Marefu
|
Na Evelyn Balozi TANGA
Wazazi
na walezi wa watoto wanao soma katika shule ya sekondari ya Semkiwa iliyopo
katika Wilaya ya Korogwe mjini, Mkoani Tanga wametakiwa kujitoa kuboresha elimu
na kuhakikisha inasonga mbele.
Hayo
yamesemwa na Mgeni Rasmi Mbunge wa Korogwe vijijini Profesa Maji Marefu katika
mahafali ya 16 ya shule hiyo kongwe Mjini hapo .
Maji
Marefu amesema baadhi ya wazazi na walezi ni wazito katika utoaji wa ada kwa
watoto,elewa kutotoa ada kwa wakati
kunarudisha nyuma maendeleo na kuondoa munkari kwa watoto kushiriki vizuri
darasani na badala yake wamekuwa wepesi kuwalaumu walimu.
Maji
Marefu amewataka wazazi kutoa ada kwa wakati kuepusha usumbufu kwa walimu na wanafunzi ili watoto
wafurahie haki yao ya msingi ambayo ni elimu.
Pia Mbunge huyo
ameuomba uongozi wa shule hiyo kuacha tabia ya kufukuzwa au kuwazuia kufanya mitihani watoto kwajili
ya ada, kwani lazima watahitaji vyeti kwajili ya maendeleo ya maisha yao walimu
wazuie vyeti hadi malipo ya ada
yakamilike.
Hata
hivyo mkuu wa shule hiyo ya sekondari Debola Singu ameeleza changamoto mbalimbali
wanazo kutananazo ikiwemo ubovu wa miundo mbinu, Uchahe wa Walimu, Ukosefu wa vifaa vya
michezo na Ukarabati wa Mahabara.
Katika
maafari hiyo Mgeni Rasmi amewapatia mipira mitatu na kutaoa ahadi ya mifuko Hamsini
ya Simenti pamoja na jezi za michezo.
No comments:
Post a Comment