Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Frasser Kashai
akizungumza na Waandishi wa Habari, (hawapo pichani)
|
Na Rebecca Duwe.TANGA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Halima Omari 65
mkulima na mkazi wa Songe mjini amefariki dunia baada yakukutwa akiwa ameuawa
kwa kunyongwa baada ya kubakwa na
kulawitiwa kisha mwili wake kutupwa kwenye korongo la takataka na watu wasiojulikana.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi
mkoani hapa Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29 octoba
mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi huko kijiji cha Songe Kata ya Songe na
Tarafa ya Kwekivu.
Kamanda Kashai amesema kufuatia msako uliofanywa
wamekamatwa watuhumiwa 3 ambao ni 1.Rashid Sulemani miaka 22 mkulima na mkazi wa
Songe mtuhumiwa huyu alikuwa ametoroka na amekamatwa akiwa wilaya ya Kiteto.
2.Kombo Kilo miaka 59 mkulima na mkazi wa
Songe , 3.Charles Mboya miaka 54 mkazi wa kijiji cha kwa Stemba.
Sambamba na hayo kamanda Kashai amesema watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili wakati wowote kuanzia sasa
baada ya upelelezi kukamilika.
Jeshi la polisi Mkoani hapa linaendelea kuwa
sisitiza wananchi kuendelea kuonyesha
ushirikiano wa kutoa taarifa za kisiri juu ya uwepo wa wahalifu katika maeneo
yao wanayoishi ili kuweza kuzuia na kukabiliana na uhalifu.
No comments:
Post a Comment