Baadhi ya Magunia ya Bangi yaliyowahi kukamatwa na Jeshi la Polisi nchini |
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na maafisa
kutoka tume ya kuthibiti dawa za kulevya wamefanya msako wa ghafla katika
vijiji vya Kisimiri na Olkokola wilayani Arumeru na kufanikiwa kukamata na
kuteketeza gunia 260 za bangi huku watuhumiwa wakidaiwa kukimbia baada ya kuona
askari hao.
Akizungumza akiwa katika eneo la operesheni hiyo iliyoanza
majira ya saa 10 alfajiri afisa kutoka tume ya kuthibiti dawa za kulevya makao
makuu January Ntisi amesema tume imeamua kuendeleza msako huo kwakuwa takwimu
zinaonesha kuwa idadi kubwa ya vijana wameathirika na dawa za kulevya ikiwemo
bangi na hii inaweza kutengeneza taifa lenye kizazi chenye tabia mbaya na
matendo ya uovu pamoja na kupunguza nguvu kazi ya taifa.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Libaratus Sabas
amesema pamoja na kuonesha kuwa kilimo cha bangi kimeanza kupungua lakini bado
wataendelea na msako na kuwataka viongozi wa vijiji vitongozi kushirikana na
jeshi katika kukomesha dawa hizo kwani wameonekana kuto toa ushikiano huku
akitoa angalizo kuwa jeshi halita mfumbia macho kiongozia atakaye bainika
kujihusisha na kulimo cha bangi.
Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamesema hata hivyo kiasi
kilicho kamatwa ni kidodo kwakuwa watu wamekuwa wajanja kwani mwaka huu wameuza
mapema kwakuwa wameshajuwa miezi inayofanywa msako na kuliomba jeshi la Polisi
libadilishe mbinu za msako wake.
Chanzo: ITV
No comments:
Post a Comment