Na
Evelyn Balozi TANGA.
Imebainika kuwa wasindikaji waliowengi nchini hawazingatii
kanuni na sheria za mamlaka ya chakula na dawa, uhifadhi na uuzaji wa vyakula
huku wengine wakiendesha shughuli hizo bila kusajiliwa hali ambayo inatia shaka
juu ya usalama wa bidhaa zao.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi Mkuu wa vyakula
kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Lazaro Mwambole katika mafunzo ya
wasindikaji wadogo wa vyakukla yanayofanyika mkoani kwa siku mbili kwenye
ukumbi wa Veta jiji Tanga.
Mwambole pia amewataka watanzania kujizoeza desturi
ya kukagua vyakuwa wakati wa manunuzi na matumizi ili kupata
Kwamujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa TFDA, ambae pia ni Meneja Ukaguzi na uthibiti wa mamlaka hiyo
Justine Makisi, amesema umuhimu wa wasindikaji wadogo kutokana na kuchangia
karibu 22% ya pato la taifa ndio uliopelekea kutolewa mafunzo hayo nchi nzima.
Tathmini ya Mamlaka ya chakula na dawa TFDA mwaka
2006/2007 ulibaini wasindikaji wadogo na wakati ambao ni asilimia 74% ya
wasindikaji waliopo nchini ambao wengi wao hawajafikia viwango vya usindikaji
salama na bora.
Hadi sasa TFDA imetoa mafunzo kwa
wasindikaji wajasiriamali 600 kutoka mikoa ya Dar es saalam, Pwani, Morogoro,
Dodoma, Singida, Arusha, Mbeya Mwanza, Mtwara, Lindi na sasa Tanga ambapo
takribani washikiri 50 watanufaika.
No comments:
Post a Comment