Na Rebeka Duwe TANGA.
Watu
wanne ambao majina yao hayakufahamika kwa haraka wanashikiliwa na jeshi la
polisi mkoani hapa kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha na kumvamia mwanamke mmoja
aliyefahamika kwa jina la Sofia Adam mkazi wa Kange wilayani Tanga mkoani hapa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda
wa polisi mkoa wa Tanga (SACP ) Frazzer Kashai amesema mnamo wa tarehe 04
Septemba mwaka huu majira ya saa 20:30 usiku huko maeneo ya Kange karibu na
chuo kikuu cha utumishi wa umma jijini hapa mwanamke huyo ambaye ni
mfanyabiashara alivamiwa akiwa Dukani kwake.
Kamanda Kashai amesema kuwa duka hilo
linalomilikiwa na Theonest Twaha ambayo ina Stetionary,na huduma mbalimbali
kama Tigo pesa ,M Pesa na Airtel money ilinyanganywa kiasi cha sh 2,000,000 ambapo watu hao
walifyatua Risasi na kufanya uhalifu huo.
Hata hivyo kamanda Kashai amesema hatua za
kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya wahalifu hao ili kuwatia nguvuni.
Katika hatua nyingine Kashai ametoa wito kwa
wakazi wa Tanga kutoa Taarifa za siri kituo chochote cha polisi kilicho karibu
za kuonekana kwa watu waliofanya tukio hilo la unyanganyi wa kutumia Silaha .
No comments:
Post a Comment