Na BBC Swahili.
Watawa
watatu wakongwe wameuawa mjini Bunjumbura katika makazi ya watawa wanawake.
Sababu
ya mauaji hayo haijulikani. Polisi wanasema kuwa wamewazuilia washukiwa wawili,
kulingana na shirika la habari la Reuters.
Watawa
hao walisemekana kuwa Lucia Pulici,mwenye umri wa miaka 75, Olga Raschietti, 82
na Bernadetta Boggian, 79.Miili yao ilipatikana wakati tofauti huku taarifa za
awali zikisema watawa wawili waliuawa.
Kwenye
mtandao wake, dayosisi ya kikatoliki ya Parma ilisema kuwa mauaji ya watatu hao
yalifanywa na mhalifu ambaye alikuwa na matatizo ya kiakili.
Watawa
hao wawili walikuwa wanashiriki kanisa katoliki la Xaverian.Mnamo mwaka
2011,mtawa mmoja na mfanyakazi wa shirika la misaada aliuawa katika tukio la
ujambazi Kaskazini ya Burundi
Burundi
ni moja ya nchi masikini amapo uchumi wake unategemea sana mapato kutokana na
Chai na Kahawa.
No comments:
Post a Comment