Kocha Mkuu wa Coastal Union,Yusuph Chippo (Kulia) akisalimia na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego mara baada ya kuwasili uwanja wa Ndege Tanga akiwa ameambana na timu hiyo wakitokea Pemba walipokuwa wamweka kambi wa kwanza kulia anayemtabulisha ni Meneja wa Coastal Union Akida Machai na kushoto ni Katibu Mkuu wa Coastal Union Kassim El Siagi,Picha KWA HISANI YA COASTAL UNION. |
Msafara wa Coastal Union ukiongozwa na pikipiki
na Baiskeli zisizokuwa na idadi wakipita katika mitaa mbalimbali jijini Tanga
kabla ya kuelekea kwenye Kambi yao iliyopo Raskazoni Jijini Tanga.
|
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege jijini Tanga mara baada ya timu ya Coastal Union kuwasili katika uwanja huo ikitokea visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi ya mwezi mmoja ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara. |
MKUU wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego leo
ameongeza mapokezi ya timu ya Coastal Union yaliyofanyika kwenye uwanja wa
Ndege jijini Tanga ambapo timu hiyo ilikuwa ikitokea Visiwani Pemba ilipokuwa
imeweka kambi kwa muda wa mwezi mzima.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo DC
Dendego amesema kuwa serikali ya wilaya hiyo haitasita kuchukulia hatua watu
wote wanaoleta migogoro na chokochoko ndani ya klabu ya Coastal Union kwa
sababu wasiposhughulikiwa wanaweza kupelekea kuwagawa wanachama,wapenzi na
mashabiki hivyo kudhoofisha maendeleo.
Wachezaji hao walitua uwanja wa ndege Tanga
wakitumia ndege mbili tofauti ambapo baada ya hapo Mkuu huyo wa wilaya aliweza
kuongoza msafara wa magari zaidi ya 50,pikipiki na baiskeli zisizokuwa na idadi
zilizunguka maeneo mbalimbali jijini Tanga huku wananchi wakijitokeza kwa wingi
kuilaki kila ilipokuwa ikipita kwa kuimba nyimbo za kuisifu timu hiyo.
Baada ya mzunguko huo ambao ulichukua
takribani saa moja ndipo wachezaji wa timu hiyo wakawasili kambini eneo la
Raskazone Hotel Pembezoni mwa bahari ya hindi ilipo kambi yao hivyo.
Dendego amesema kuwa lazima wao kama serikali
wahakikisha klabu zao mkoani hapa zinakuwa na utulivu kila wakati kwa hiyo
inapotokea inakwenda kunyume chake basi wao watachukua hatua kali ili iweza
kuwa fundisho kwa watu wengine ambao wanaweza kufanya hivyo kipindi kingine.
Hata hivyo amesema kuwa lazima wapenzi
,wanachama na mashabiki kuhakikisha wanakuwa na mshikamano wa thati ili kuweza
kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake waliojiwekea kwenye msimu mpya wa
Ligi kuu soka Tanzania bara.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Coastal
Union,Kassim El Siagi amesema kuwa timu hiyo ilifanya usajili mzuri msimu huu
hivyo wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwa kuanzia na mechi yao na
Simba ambao haiwapi wasiwasi wa aina yoyote ile.
El Siagi amesema kutokana na maandalizi timu
hiyo walioifanya wakiwa visiwani Pemba wana matumaini makubwa ya kuibuka na
pointi tatu muhimu mbele ya Simba mechi ya ufunguzi wa Ligi kuu itakayochezwa
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Awali akizungumza katika mapokezi
hayo,aliyekuwa Mwenyekiti wa Coastal Union,Hemed Aurora amewataka wapenzi
,wanachama kudumisha na kuendeleza mshikamano ili kuiwezesha timu hiyo kuweza
kufikia malengo yao ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao.
“Umoja na mshikamano ndio siri ya mafanikio
yoyote yale hivyo nawasihi wapenzi ,mashabiki na wanachama muenzi mshikamno kwa
sababu ndio nuru ya mafanikio kwenu “Alisema Aurora.
No comments:
Post a Comment