HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 16 September 2014

WATU WAISHIO NA KISUKARI NA BP PEMBA WAHIMIZWA KUFANYA MAZOEZI NA KULA MATUNDA


Na Masanja Mabula.Pemba
Jamii inayoishi na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu (presha) imehimizwa kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi pamoja na kutumia vyakula vya matunda na mboga mboga  ili kukabiliana na magonjwa hayo ambayo yanasababishwa ulemavu wa maisha na vifo vya watu wengi .

Akitoa ushuhuda kwa madiwani na masheha wa Wilaya ya Micheweni Bi Jokha Zaharani ambaye ni mgonjwa wa Kisukari amesema kuwa bado jamii inawatenga wagonjwa wa Kisukari kwa kuwapa chakula ambacho hakina virutubishi vinavyohitajika kwa ajili ya kujenga afya zao .

Amesema kuwa mgonjwa wa Kisukari anatakiwa kuishi kama mtu mwengine katika ulaji , licha ya kwamba mgonjwa wa Kisukari anamahitaji sawa na mtu wa kawaida na kufahamisha kwamba mgonjwa wa kisukari anatakiwa kula matunda na mboga mboga .

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya Zanzibar Omar Mwalimu Omar ameitaka jamii kuwa na utamaduni ya kupima afya mara kwa mara pamoja na kufuata ushauri wa wataalmu pindi wanapobainika kuwa na ugonjwa wa kisukari na presha.

Aidha amesisitiza haja kwa jamii kuchukua tahadhari na mapema za kujikina na ugonjwa wa Kisukari ikiwa ni pamoja na kudhibiti msongo wa mawazo , kujiepusha na utumiaji wa pombe , sigara na tumbaku sambamba na kufanya mazoezi mara kwa mara.

Mapema akifungua mkuatano huo Afisa Tawala Wilaya ya Micheweni Hemed Khalid Abdalla amewataka madiwani na masheha kutumia vikao vyao pamoja na kamati zao kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuchungua afya zao katika Vituo vya afya ili wapatiwe tiba sahihi watakaopatikana na magonjwa hayo .

No comments:

Post a Comment