HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 16 September 2014

INASIKITISHA.! "MAHABUSU YA WATOTO TANGA YAISHIWA CHAKULA"



Mkuu wa Mkoa wa Tanga .Luteni Mstaafu Chuku Galawa(Picha na Maktaba)
Na Eveln Balozi TANGA.
‘UONGOZI wa idara ya Ustawi wa jamii mkoani Tanga, inahaha kutafuta chakula kwa wahisani mbalimbali mkoani hapa, kunusuru watoto wadogo chini ya umri wa miaka 18 waliowekwa katika mahabusi iliyopo barabara 15 Jijini Tanga, wasilale na njaa kutokana na kambi hiyo kuishiwa chakula tangu Alhamisi ya wiki iliyopita.

Hali hiyo imejitokeza baada ya Huruma fm kufika katika kituo hicho, kufuatilia suala la kukosekana kwa huduma ya maji ambayo yamekatwa kufuatia mahabusi hiyo kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 1 na Mamalaka ya Majisafi na Majitaka (Tanga-Uwasa).

Mkuu wa mahabusi hiyo Clara Kibanga alisema pamoja na kuwepo changamoto ya ukosefu wa maji katika kituo hicho na kwamba hakuna kabisa jitihada zinazofanywa kurejesha, lakini pia kumejitokeza tatizo jingine la kuishiwa chakula kwa watoto hao hatua ambayo hawajui kuanzia leo Jumatatu watoto hao watakula nini.

"Maji hayajarudishwa hadi sasa na pia hivi unavyoniona naenda mkoani kwa Ofisa wetu wa mkoa kuangalia uwezekano kama naweza kupata chakula maana chakula kilichokuwepo kimeisha tangu jana (Jumamosi), hatujui watoto leo watakula nini," alisema Mkuu wa mahabusi hiyo.

Alisema katika mahabusi hiyo watoto wanane waliopo hawana chakula kama mchele, unga, sukari, chumvi, mafuta na maharage hatua ambayo hawajui tatizo hilo ufumbuzi wake utatauliwa lini na serikali kutokana na kwamba wamekuwa wakitegemea wafadhili ambao si mara zote wamekuwa wakifika hapo.

Ofisa Ustawi wa Jamii mkoani Tanga Emanuel Simpungwe, alipoulizwa kuhusiana na hali hiyo, alikiri mahabusi hiyo kukosa chakula na suala la maji licha ya serikali kueleza kwamba wangetuma fedha za kutatua matatizo hayo.

Alisema kwamba siyo mahabusi hiyo pekee inayokabiliwa na matatizo hayo lakini pia kambi ya wazee iliyopo Mwanzange Jijini Tanga na kambi nyingine ya wazee iliyopo Msufini wilayani Muheza imekuwa pia ikikabiliwa na tatizo na uhaba wa chakula.

"Ni kweli mahabusi ya watoto haina chakula lakini siyo hiyo tu hata kule kwa  wazee wasiyojiweza Mwanzange na Misufini Muheza nako hakuna chakula tunawasubiri wenzetu huko Wizarani watuletee fedha tuweze kutatua changamoto hizi," alisema Simpungwe.

Serikali kupitia msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Nsachris Mwamwaja, alisema serikali inafanya jitihada kuhakikisha wanatatuza changamoto hizo katika mahabusi hiyo na sehemu nyingine ya vituo vilivyopo chini ya wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment