Na Rebeca Duwe
Mtu mmoja
aliyetambulika kwa jina la Ngowa Mwero mwenye umri wa miaka 50 mkaazi wa kijiji
cha Ng’ombeni Wilayani Mkinga mkoani hapa, ameuwawa na watu wasiofahamika baada
ya kushambuliwa kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hile
limetokea mnamo Sep 16 mwaka huu majira ya saa 7 na nusu usiku ambapo mtu huyo
ambaye ni Mganga wa kienyeji alivamiwa na watu hao wenye silaha na kushambuliwa
kwa Mapanga Kichwani mgongoni na kwenye mkono wake wa kushoto.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Freizer Kashai amesema chanzo cha
tukio hilo ni Imani za kishirikina na hakuna aliyekamatwa mpaka sasa kuhusiana
na tukio hilo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi ilibaini wahusika
wa Mauaji hayo.
Aida Kamanda Kashai
anatoa wito kwea Jamii kuacha kujichukulia Sheria mkononi kwani ni kosa
kisheria na ni Uhalifu kama uhalifu mwingine.Mwili wa Marehemu umehifadhiwa
katika hospitali ya Rufaa Bombo.
No comments:
Post a Comment