Kamanda Kashai |
Na Pamela Chaula.TANGA
Jeshi la Polisi
Mkoani hapa linawashikilia watu 27 raia wa Ethiopa kwa kuingia nchini bila
kibali na wanne kati yao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa Bombo kutokana na
kudhoofu kwa njaa.
Watu hao
wamekamatwa katika Matukio mawili tofauti ambapo katika tukio la kwanza
wamekamatwa wahamiaji haramu wawili(2) wakiwa ndani ya Gari lenye namba za
Usajili T 147 BWN Scania mali ya Kampuni ya Simba Mtoto wakiwa wameingia nchini
bila kibali.
Katika tukio la
pili wahamiaji haramu 25 wamekamatwa
kwenye Pori la Saruji katika kata ya Pongwe wakiwa wameingia nchini bila kibali
ambapo wanne kati yao wamelazwa Hosptali ya Bombo kutokana na kudhoofu kwa
njaa.
Waliolazwa
wametambuliwa kwa majina Mubarik Jamal 18,Muhamada Jama 25, Dejene Ashore 19,
na Tendere Daviel Awawo 18.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Tanga Fresser Kashai anatoa wito
kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Wananchi wote kuwatambua wageni
wote wanaoingika katika maeneo yao na Pindi wanapowatilia shaka kuwa sio raia
wa Tanzania au ni wahalifu wawatolee taarifa mapema katika vituo vya Polisi.
No comments:
Post a Comment