Viongozi wa dini nchini wametakiwa kutumia
karama ya utumishi wao kuwashauri na kuwaonya wanaojihusisja na vitemdo vya
dhuluma dhidi ya wanyonge kwani kwa kufanya hivyo wanawakosesha haki zao na ni
kinyume na mpango wa mungu.
Rai hiyo imetolewa na Padre Hodelo Shedafa
kwenye adhimisho la ibada ya misa takatifu kwenye kanisa la Mt. Anthoni wa
Padua Chumbagani, Jimbo Katolili la Tanga.
Amesema niwajibu kwa viongozi kutenda haki
kwa wote pasipo kuwakandamiza na ubinafsi bali kufanya mabadiliko yakweli
ambayo yatalifanya taifa kuwa na amani na upendo kwa wote.
Samba na hayao Waumini wa kanisa katholiki
jimbo la Tanga wametakiwa kudumisha upendo na amani na kudumu katika imani yao
ya kumtumaini mungu wa kweli na kuachana na
mambo ya ulimwengu huu kwani mwisho wa yote lazima warudi kwa mungu na
kuiacha dunia kama ilivyo.
Hayo yamesemwa na Padre Richard Munyau
Mwanzia katika ibada ya misa takatifu ya kumkumbuka somo wa jumuiya ya mt.
agustino kichangani maweni parokia ya mt. Petro saruji.
Hata hivyo amewaasa wazazi kuziombea familia
zao hususani watoto kwa kuiga mfano wa mtakatifu Monika mama yake na mtakatifu
Agustino ambaye alimlea katika maadili mema na hata kufa mtakatifu mwafrika.
Padre Mwanzia amewataka waumini hao kuacha
uadui kati ya mtu na mtu na badala yake waombeane na kuwakumbuka wenye shida
mbalimbali katika jamii.
No comments:
Post a Comment