Kamanda wa
polisi mkoani Tanga kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la Polisi Frasser Kashai
(wa pili kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari akionesha Mirungi hiyo
katika Mafungu.
|
Na Pamela Chaula.Tanga
Jeshi la polosi
mkoani hapa linamshikilia Mtu mmoja mkazi wa Sahare Ally Ramadhani (33) kosa la kukamatwa na mirungi katika eneo la
Kiomoni wilayani Tanga mnamo tarehe 2 sep mwaka huu.
Kamanda wa polisi
mkoani Tanga kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Frasser Kashai amethibitisha kukamatwa kwa kgs 68 iliokuwa kikisafirisha na pikipiki
yenye namba za T 906 CBT aina ya Sunlg nyekundu majira ya saa 4:00 usiku na
askali polisi waliokua doria.
Kamanda wa polisi
mkoani hapa ametoa wito kwa wanaojihusisha na uuzaji au matumizi ya madawa ya
kulevya kuacha mara moja kwani ni ukiukwaji
wa sheria ya nchi.
Pia kamanda
amewataka wananchi kushilikiana na jeshi la polisi kuwafichua wale
wanaojihusisha na uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya kwani uathiri nguvu kazi ya Taifa na kuzorotesha maendeleo
kwa ujumla.
Wakati huo huo
kamanda kashai ametoa wito kwa wananchi wakaao maeneo ya jirani na mipaka wa
Tanzania na nchi jirani ya Kenya kutokufumbia macho wa hamiaji haramu wapitao
katika njia za panya.
Kamanda kashai
amesema yeyote anayepokea na kuwaifadhi waamiaji haramu anakiuka sheria ya nchi
na akibainika atachukuliwa hatua za kisheria ,wananchi waache tabia ya
kuwahifadhi watu tuwasio wajua ndiyo wanaosababisha uhalifu katika nchi yetu.
No comments:
Post a Comment