Mshambulaji
wa Coastal Union aliyesajiliwa kutoka timu ya Gormahia ya Kenya Itubu Imbem kushoto akiwa na Meneja wa timu ya Coastal Union,Akida Machai mara baada ya kusaini mkataba wa miaka
mwii wa kuitumia timu hiyo
hivi karibuni
|
Falcon Fc
inashiriki Michuano ya Ligi daraja la kwanza visiwani humo ambapo
ilikutana na dhahama hiyo ya mabao kutoka kwa wachezaji mahiri ambao wamesajiliwa msimu
mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Wakionekana
kujiamini na kujipanga vilivyo,Coastal Union waliweza kuendeleza wimbi la
mashambulizi langoni mwa wapinzani wao hao na kufanikiwa kupata mabao hayo
ambapo mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko Coastal Union walikuwa mbele kwa
mabao 5-0.
Mabao ya Coastal
Union mengine yalifungwa na Abasi Athumani ambaye alipachika mabao matatu
kwenye mchezo huo wakati Mahundi Petro na Mbwana Hamisi kila mmoja akipachika
bao moja langoni mwa timu hiyo.
Katika kuhakikisha
Coastal Union inaendelea kuibuka na idadi kubwa ya mabao iliweza kuendelea kasi
ya mashambulizi langoni mwa Falcon na kufanikiwa kuandika mabao mengine ambapo
Rama Salim mchezaji mahiri naye aliyetokea klabu ya Gormahia ya Kenya ambaye
pia aliwahi kuichezea Harambee Stars ya nchi hiyo aliweza kuandika mabao mawili
na kuhitimisha karamu ya mabao.
Akizungumzia hali
ya kikosi hicho,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Yusuph Chippo alisema kuwa kutokana na
maandalizi waliyoyafanya wakiwa visiwani humo wanamatumaini makubwa ya kufanya
vizuri katika michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara itakayoanza Septemba 20
mwaka huu.
“Ninaweza kusema hivi kuwa sasa kikosi changu kimeimarika kwani hapo juzi
tuliifunga timu ya Opec ya Visiwani hapa mabao 11-0 hivyo kikosi changu
kipo tayari kushiriki michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao na
hasa tukianzia na mechi yetu na Simba kwa kuchukua pointi tatu muhimu “Alisema
Chippo.
No comments:
Post a Comment