Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh Halima Dendego(Picha na Maktaba) |
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh Halima Dendego
amemwomba mstahiki wa meya jiji la Tanga pamoja na wakuu wa idara
zote za halmashauri zikiwemo idara ya vijana ,kitengo cha ukimwi na watu wa mashirika
waone umuhimu wa kuwatunza wanamgambo na kuwapa mafunzo ambayo yatawafanya wawe na akili
timamu ili kuondokana na hali ya umaskini.
Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo katika
ufunguzi wa mafunzo ya wana mgambo ambao umefanyika katika viwanja vya
wanamgambo lilipo maeneo C A C Gofu mkoani hapa.
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yanawaandaa
vijana kuwa wakakamavu , watimilifu na kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri hasa kwa ajili ya ulinzi na
usalama wa nchi yetu.
Sambamba na hayo Mh Dendego amewaahidia vijana
hao kuwa atwaandalia somo la stadi za maisha
ambalo litawasaidia katika maisha yao ili wawe na akili nzuri na kuwa imara
katika kazi zao na watakapo maliza mafunzo yao wajue jinsi ya kutoka kiuchumi
na katika uaskari wao.
No comments:
Post a Comment