Askofu Anthony Banzi wa Jimbo Katoliki la Tanga |
Na Dominic Maro. Tanga
Wito umetolewa kwa Wakristu wote nchini kutenda mema
kila wakati siyo kupenda kutenda maovu ambayo ni chukizo machoni pa MUNGU wetu.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Anthony Banzi wa Jimbo Katoliki la Tanga kwenye adhimisho la
ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika kanisa kuu la Mtakatifu Anthony wa
Padua parokia ya Chumbageni Tanga ibada hiyo ilikuwa ni maalum kwa umoja wa
wanawake wakatoliki Tanzania (wawata) jimbo la Tanga kumshukuru mungu kwa kumaliza
mkukutano wao mkuu na kumuomba awajalie baraka.
Askofu banzi amesema kila mmoja wetu akitenda mema
au maovu ndiyo atakavyo hukumiwa kulingana na aliyotenda,hivyo tufuate mfano wa
bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametufundisha upendo na kuishi ukweli daima
milele.
Hata hivyo Mhasham Askofu Banzi hakusita kuwakumbusha
Wanawake Wakatoliki kuwa umoja wao ni muhimu sana kwa kuendeleza kazi ya kitume
kwa kutangaza kazi ya MUNGU na kila mwanamke mbatizwa anaingia moja kwa moja
katika kazi hiyo ambayo tumekabidhiwa sisi sote.
No comments:
Post a Comment