HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 21 September 2014

UBINAFSI WAWAPONZA VIONGOZI WA KIJIJI CHA PONGWE KASKAZINI, MKUU WA WILAYA AWABURUZA KORTINI KWA UBADHILIFU.

Baadhi ya Wanafunzi wa Pongwe Sekondari.

Viongozi wa Jiji na Mkoa wa Tanga wakiwa katika ziara kwenye kata ya Pongwe. Kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe Mwana Uzia,Meya wa Jiji la Tanga Mh Omar Guledi,Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mh Halima Dendego na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa.(Alies imama)

Baadhi ya Wakaazi wa Pongwe
NA REBEKA DUWE. PONGWE. 
Wananchi wa Mkoani hapa wametakiwa  kuacha tabia ya  kuvunja sheria kwa kuchukua maamuzi yao binafsi ya  kuuziana viwanja bila kufuata utaratibu uliowekwa kisheria ili kuepukana na migogoro mbalimbali inayojitokeza baina yao hususani ugwaji wa viwanja.

Hayo yamesemwa na Afisa Tarafa wa tarafa ya Pongwe wilayani Tanga Mkoani hapa, bw.Juma Msagati wakati akizungumza na Redio Huruma akiwa ofisini kwake kuhusiana na wajumbe tisa wa viongozi wa serikali ya kijiji cha Pongwe kaskazini kufikishwa kituo cha polisi  tarehe 7 Septemba kwa tuhuma za kuuza viwanja ambavyo vimetengwa kwa ajli ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Pongwe.
Afisa huyo amesema kuwa wajumbe hao walipelekwa kituoni kwa Amri ya mkuu wa wilaya kwa ajili wakati akifuatilia utekelzaji wa ugwaji wa viwanja na migogoro wa mipaka ambayo mara nyingi imekuwa ni changamoto kubwa katika tarafa ya Pongwe na kusababisha migogoro mara kwa mara.
Aidha Tarafa ya Pongwe ina jumla makazi 79 , na vijiji 13, na mitaa 30 vilevile vitongoji 59 ambapo kata zilizopo ni kata ya Pongwe,Maweni ,Marungu Duga,Tanga sisi ,Airpot na kata ya Tongoni ambazo karibu zote hizo zimeshuhudiwa kuwa na migogoro ya ardhi.

Hata hivyo amewashauri wanachi wote wanaoishi mipakani ambao wanataka kujenga wasiendelee kujenga mpka pale watakapo baini mipaka yao ili wasiendelee kupata migogoro isiyo ya lazima lakini pia amesema endapo kutatokea suala kutokutosha kwa ardhi wawaonene watu wa mipango miji badala kuvamia ardhi bila utaratibu.

Sambamba na hayo Msagati ameto wito kwa wafugji pamoja na wakulima kufanya kazi kwa bidii na kufuga mifugo kwa maarifa ili kuweza kufikia mafanikio yao .

No comments:

Post a Comment