Mwanafunzi mwenye Ujauzito(Picha na Maktaba) |
Na Masanja Mabula Pemba
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamtafuta kijana
anayehusika na ujauzito wa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika skuli ya
sekondari ya Wete aliyejifungua na kisha kumtupa mtoto ndani ya shimo la choo .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini
Kamishina msaidizi Pemba shekhan Mohammed Shekhan amesema kuwa tukio limetokea
septemba 26 majira ya saa mbili za asubuhi huko Finya katika Wilaya ya
Micheweni .
Amesema kuwa tayari jeshi hilo
linamshikilia mwanafunzi huyo Ziana Khamis Ali (18) ambaye anatuhumiwa kuhusika
na tukio la kikatili na kwamba kwa sasa anahojiwa ili aweze kufikishwa
mahakamani kujibu tuhuma zinamkabili .
Sheha wa shehia ya finya omar ali
Omar amefahamisha kwamba mwanafunzi huyo alibainika baada ya uongozi wa Shehia
kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi kuanza kuwafanyia uchunguzi wasichana
wanaoishi nyumba za jirani na eneo la tukio ambapo mhusika alitoroka kwa lengo
la kutaka kukimbia .
Amesema kuwa kitendo cha kuzaa mtoto
na kisha kumtupa ni kwenda kinyume na misingi ya haki ya binadamu na kueleza
kuwa kichanga hicho kilikuwa na haki ya kuishi na kupata haki zote stahiki kwa
mujibu wa msingi hiyo .
Wakizungumza na mwandishi wa habari
hizi katika eneo la tukio baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa
mwanafunzi huyo alikuwa ni miongoni mwa wanajamii waliokuwa wanashughulika
kukitoa kichanga hicho ndani ya shimo kana kwamba yeye sio mhusika wa tukio
hilo
Hata hivyo taarifa z aidi
kutoka kwa wanafunzi wenzake wanasema kuwa siku ya alkhamis walikuwa pamoja na
skuli na hawakufahamu kwamba mwenzao anaujauzito wa miezi tisa.
No comments:
Post a Comment