HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 27 August 2014

WAKAZI WA HANDENI TANGA WAKAMATWA NA BANGI ZANZIBAR.



Na Masanja Mabula –Pemba.
Wakaazi wa wawili  Kisosora Wilaya ya Handeni Mkao wa Tanga wanashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kosa la kupatikana wakiwa na majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi .

Tukio hilo limethibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohammed Shekhan Mohammed ambaye amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mahidia Othman Suleiman (46) na Sauda Amir Msisi (26) .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda Shekhan amesema kuwa akinamama hao walikamatwa na jeshi la Polisi  siku ya jumanne muda mfupi baada ya kushuka katika bandari ya Wete wakitokea Tanga  wakiwa kwenye chombo chenye jina Royal .

Amesema kuwa askari wa jeshi hilo waliwatilia mashaka akinamama hao na baada ya kufanya upekuzi kwenye bagi yao walibaini kuwemo na mafurushi 21 ya majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi yakiwa yamehifadhiwa kwenye kiroba chini ya nguo zao .

Aidha kamanda Shekhan amesema kuwa baada ya kufikishwa katika kituo cha Polisi mtuhumiwa Mahadia alijaribu kuwakimbia askari lakini kutokana na umahiri wa  askari walifanikiwa kumtia katika himaya yao kabla ya hajafika mbali .

Ameeleza kwamba baada ya kuhojiwa walisema kwamba wanamwenyeji wao katika Shehia ya Mjimbini Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba ambaye anafahamika kwa jina la Khamis Mwanamarando .

Hata hivyo akinamama hao wamesema kuwa mzigo huo hauwa ni mali yao bali wamebadilishiwa begi yao kutokana na begi hilo  kufanana , ambapo mzigo wao umepotea ndani ya chombo hicho .

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili pindi upelelezi utakapo kamilika .

No comments:

Post a Comment