HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 27 August 2014

BEKI MBWANA KIBACHA WA COASTAL AM'BEZA COUTINHO WA YANGA NA KUSEMA ANAKABIKA.


Mbwana Bakar Kibacha

Na Masanja Mabula -Pemba.
Beki kisiki wa Timu ya Coastal Union ya Tanga Mbwana Bakar Kibacha amebeza kiwango cha mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga Mbrazil Andrew Continho na kusema kuwa mshambuliaji huyo  anakabika .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kisiwani Pemba Kibacha amesema kuwa mshambuliaji huyo ni kawaida na  hana tofauti na wachezaji wa hapa nchini na kuongeza kuwa tofauti iliyopo ni kwamba anatoka nchini Brazil .

Amesema kuwa kiwango alichoonyesha mshambuliaji huyo kwenye mchezo wa kirafiki kati ya timu yake na Chipukizi uliochezwa katika uwanja wa Gombani ni cha kawaida na kwamba hawezi kumpa presha .

"Ni mchezaji wa kawaida tu na hana tofauti na wachezaji wa hapa nchini , lakini kabla ya kumuona nilikuwa nikisikia kwenye vyombo vya habari , kumbe mweppesi na anayekabika kiurahisi "alifahamisha Kibacha.

Aidha Kibacha ambaye pia ni nahodha wa wagosi wa Kaya alivitaka vyombo vya habari kuacha kuwapamba wachezaji bali waandike na kutangaza sifa na uwezo  alionao mchezaji na sio kuonghezea chumvi kwa lengo la kufanya biashara katika vyombo vyao.

Katika hatua nyingine mlinzi huyo wa kati wa Wagosi wa Kaya amesifu usajili uliofanywa na uongozi wa timu hiyo na kuwataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono ili lengo lao la kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu.
"Usajili uliofanywa kwa kweli umenipa matumaini ya kuwafanya vyema kwenye ligi kuu msimu , cha msingi ni mashabiki na wapanzi wa klabu kuendelea kuinga mkono klabu ili iweze kufanikisha azma ya kutwa ubingwa wa ligi kuu msimu huu " alisisitiza.

Timu ya Coastal Union ya Tanga iko Kisiwani Pemba kwa ajili ya kambi ya siku ishirini 20  mazoezi kujiandaa na ligi ya Vodocom Tanzania Bara ambayo imepengwa kuanza kutimua vumbi  Septemba 20.

No comments:

Post a Comment