UEFA jana imempa Tuzo yao ya
Mchezaji Bora wa Mwaka Cristiano Ronaldo baada ya kuwabwaga kwenye Kura Kipa wa
Mabingwa wa Dunia Germany, Manuel Neuer na Mchezaji mwenzake wa Klabu ya Bayern
Munich anaechezea Holland, Arjen Robben.
Ronaldo, Miaka 29, alifunga Bao 17
katika Mechi 11 za Ulaya wakati Real Madrid inaelekea kutwaa Taji lao la 10 la
Ulaya walipobeba Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia kuisaidia Klabu yake
kutwaa Copa del Rey Msimu uliopita huko Spain.
Baada ya kukabidhiwa Tuzo yake, Ronaldo alisema: “Nimefurahi kweli kweli. Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”
Baada ya kukabidhiwa Tuzo yake, Ronaldo alisema: “Nimefurahi kweli kweli. Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”
Awali Majina ya Wachezaji 35
yalipigiwa Kura na kubakia 10 na kutangazwa hapo Julai 18 na kisha kubakishwa
Matatu ambayo hii Leo ndio Mshindi kapatikana.
++++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern
Munich]
++++++++++++++++++++++++++++++
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la
Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka
2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya
Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji
Bora wa Mwaka kwa Klabu.
LISTI YA WAGOMBEA 10:
-Diego Costa
-Angel Di Maria
-James Rodriguez
-Luis Suarez
-Philipp Lahm
-Thomas Muller
-Manuel Neuer
-Arjen Robben
-Cristiano Ronaldo
-Lionel Messi.
Hizi
Ni Tuzo Alito Twaa Kwa Mwaka Huu Tu..!
|
No comments:
Post a Comment