HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 31 August 2014

MAFUNZO NAMNA YA KUKABILIANA NA EBOLA YATOLEWA MWANZA




Na Lodrik Ngowi.MWANZA
Mafunzo juu ya ugonjwa wa ebola yameanza kutolewa mkoani Mwanza
mwishoni mwa wiki iliyopita, lengo likiwa ni mikakati ya serikali ya
kujiandaa na kuweka mazingira mazuri ya kuweza kukabiliana na ugonjwa
huo licha ya kwamba mpaka sasa hakuna mtu anayesadkiwa kugundulika na
virus vya  ugonjwa huo mkoani hapa.

Mafunzo hayo mkoani hapa  yalichelewa  kuanza kutokana na wajumbe wa
mafunzo hayo kudai kutopewa fedha za kujikimu,chai chakula na usafiri.

Hali hiyo ilitokea baada ya kupewa taarifa kabla ya kuanza juu ya kila
mtu atatakiwa kujigharamia mwenyewe chai  na chakula hatua iliyofanya
wajumbe hao wahoji  juu ya suala hilo la kuendesha mafunzo hayo pasipo
kuwepo na namna ya kuwawezesha.

“Wengine tumetoka mbali hatuna hata fedha hata za chai tukitegemea
kwamba tutawezeshwa huku , kwakweli ni jambo la kusikitisha kuona
kwamba tunafika hapa tunaambiwa kuwa hata chai na chakula tujitegemee
haituingii akilini”alisema mmoja wa wajumbe hao huku akiungwa  mkono
na wajumbe wote.

Naye mjumbe mwingine alisema“Itakuwaje kiandaliwe kitu muhimu kama
hiki alafu ishindikane kuwawezesha wajumbe angalau hata kwa chai,hili
inaonesha kutokuwa makini juu ya jambo hili kwani hata
tutakayofundishwa hapa yanaweza yasizingatiwe  maana watu wanaweza
kushindwa kuwa makini kwa kile kitakacho kuwa kinafundishwa na
ukizingatia hili ni suala muhimu linagusa maisha ya watanzania”

Katika mafunzo hayo ya siku moja juu ya kukabiliana na ugonjwa wa
Ebola yalitolewa kwa  waganga wakuu wa wilaya na wajumbe wa timu ya
kukabiliana na majanga ya hospitali za wilaya za
Magu,Misungwi,Kwimba,Nyamagana Ilemela,Ukerewe na Sengerema.

Akitoa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya mratibu wa magonjwa ya
dharura mkoani Mwanza Charles Bundu alisema kuwa ugonjwa huu wa ebola ni hatari na mbaya sana kuliko inavyodhaniwa.

 “Ugonjwa huu wa ebola ni mbaya sana ni zaidi ya majanga
tuliyozoea,kwa mtu ambaye ana virusi hivi ni rahisi sana kumuambukiza
mwingine  na mbaya zaidi bado tiba yake haijapatikana,hivyo yatupasa
kuwa makini nao”alisema na kuongeza :

“Tunawafundisha namna ya kuweza kujikinga na ugonjwa huu na njia
sahihi  mtakazoweza kutumia wakati ukimuhudumia mtu anayesadikika kuwa
na ugonjwa huo ili kujilinda wewe na wengine pia elimu hii mwende
mkawafundishe wahudumu wa afya huko kwenye wilaya zenu”

Bundu alifafanua kuwa miongoni mwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na
homa kali,kuumwa kichwa,kutapika mfululizo na kuumwa kifua,huku
akitahadharisha kutoshikana mikono na kumgusa mtu anayesadikiwa kuwa
na ugonjwa huo badala yake watoe taarifa kwa kituo chochote cha afya
kilichokaribu.

Aidha  alisema kwa  Mwanza tayari eneo la kuwahudumia wagonjwa hao
limeisha tengwa na hatua za kuliboresha zinaendelea pindi atakapokuwa
amapatikana mgonjwa wa ebola,eneo lililotengwa ni Huduma shuleni.

Hata hivyo inachukua muda wa wiki tatu kuweza kujiridhisha kama mtu
aliyechukuliwa vipimo vya ugonjwa huo kama ameambukizwa au
hajaambukizwa.

No comments:

Post a Comment